Albrecht Dürer

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dürer alivyojichora mwenyewe mnamo 1498

Albrecht Dürer (21 Mei, 1471 - 6 Aprili, 1528) alikuwa mchoraji na mkata nakhshi Mjerumani. Alifahamika pia kama mtaalamu wa hisabati hasa jiometria. Ahesabiwa kama msanii muhimu zaidi wa zama ya mwamko katika Ulaya ya kaskazini.

Yaliyomo

[hariri] Mitindo ya kazi

Sehemu kubwa ya kazi za Dürer ni chapisho za picha nakhshi katika ubao au shaba. Alichora pia picha kwa rangi za mafuta na rangi za maji.

[hariri] Maisha

Dürer alizaliwa mjini Nürnberg alipoishi na kufa. Wakati ule Nürnberg ilikuwa mji tajiri wa biashara ya kimataifa. Baba yake alikuwa Mhungaria aliyemfundisha ufundi wa kuchonga dhahabu. Alipokuwa kijana alifanya matembezi ya miaka mitano katika Ujerumani, Uholanzi na Uswisi alipoboresha sanaa yake. Baadaye aliongeza safari ya kwenda Italia alipofanya kazi Venezia na kuona mengi.

1494 alifunga ndoa na Agnes Frey akafungua karakana yake. Kazi mashuhuri ya kwanza ilikuwa mfululizo wa picha nakhshi katika ubao 15 kuhusu ufunuo za Yohane.

Aliendelea kuchora picha nyingi za kidini juu ya hadithi na watu wa Biblia. Lakini alitafutwa pia na matajiri na wakubwa waliotaka picha yao. Kuanzia 1512 aliajiriwa mara nyingi na Kaisari Maximilian I.


[hariri] Picha

[hariri] Viungo

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: