Actors Studio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Coordinates: 40°45′36″N 73°59′34″W / 40.760068°N 73.992654°W / 40.760068; -73.992654

Jengo la Actors Studio huko West 44th Street mjini Manhattan, -mebadilishwa kuwa kanisa.

Actors Studio ni shirika la uwanachama kwa ajili ya waigizaji wa kulipwa, waongozaji wa tamthilia na waandishi wake katika 432 West 44th Street mjini Clinton karibia na Manhattan huko New York City. Shirika lilianzishwa mnamo tar. 5 Oktoba 1947, na Elia Kazan, Cheryl Crawford, Robert Lewis na Anna Sokolow ambaye ndiye aliyefundisha harakati za waigizaji kuwa wanachama.[1] Lee Strasberg alijunga baadaye na kuchukua uongozi mnamo 1951 hadi kifo chake kunako 17 Februari 1982. Kwa sasa shirika linaendeshwa na Al Pacino na Ellen Burstyn. Studio hii ni mashahuri sana kwa kazi zake za kuboresha na kufundisha namna ya kuigiza. Wazo hili lilitokana na Group Theatre kunako miaka ya 1930 kulingana na uvumbuzi wa Constantin Stanislavski. Wakati katika Studio, waigizaji wanafanya kazi pamoja ili kukuza maarifa yao katika hali ya kujitegemea, ambapo wanaweza wakachukua hatua kama waigizaji bila kupata msukumo wowote wa kujihusisha na masuala ya kibiashara.

Kundi hili walikuwa wakifanyia mazoezi yao katika sehemu ya Princess Theatre [2] Mwaka wa 1955 wakahamia katika sehemu yao ya sasa ambapo zamani kulikuwa eneo la kanisa la Wasabato, -mejengwa mnamo 1859.[3]

Mwaka wa 1965 Actors Studio wamefungua tawi lao huko katika pwani ya magharibi mjini West Hollywood, California. The Actors Studio West inaendeshwa na uongozi wa kisanii-kiongozi ambapo kuna Mark Rydell na Martin Landau na ni tawi rasmi pekee la Actors Studio duniani.

Muundo[hariri | hariri chanzo]

Rais[4]

Viongozi Wasanii (New York):[4]

Wahitimu maarufu[hariri | hariri chanzo]

Kulingana na historia yake ndefu ya kutoa waigizaji mashuhuri na wenye mafanikio, waongozaji na waandishi waliotokana na studio, ni pamoja na:[5][6]

Soma zaidi[hariri | hariri chanzo]

  • A Method to their Madness: The History of the Actors Studio, by Foster Hirsch. Da Capo Press, 1986. ISBN 0306802686.
  • The Actors Studio: a History, by Shelly Frome. McFarland, 2001. ISBN 0786410736. cassandra morency

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Actors Studio kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.