Aachen
| Aachen | |
| Ukumbi wa manisipaa ywa wa Aachen. | |
| Mahali pa Aachen katika Ujerumani | |
| Anwani ya kijiografia: 50°46′31″N 06°04′58″E / 50.77528°N 6.08278°E | |
| Nchi | Ujerumani |
|---|---|
| Jimbo | Rhine Kaskazini-Westfalia |
| Idadi ya wakazi (2009) | |
| - Mji | 258,380 |
| Tovuti: http://www.aachen.de/ | |
Aachen (tamka: akhen) ni jiji nchini Ujerumani na lipo katika jimbo la Rhine Kaskazini-Westfalia. Mji una wakazi wapatao 260,000 wanaoishi katika mji huo na pia mji unajulikana kwa kuwa na chuo kikuu cha Rheinisch-Westfälisch Technische Hochschule (RWTH) na kuwa na historia nzuri ya kuanzia mwanzoni mwa Zama za Kati.
[hariri] Historia
Chanzo cha Aachen kilikuwa chemchemi za maji moto zilizotumiwa na watu kama tiba ya maradhi mbalimbali. Waroma wa Kale walijenga bafu hapa kwa jina la Aquis-Granum maana yake maji ya mungu ya tiba aliyeitwa Granus. Karolo Mkuu alipenda kuja hapa akaagiza kujengwa kwa mji kamili akaifanya kuwa mji mkuu wake akaipamba kwa kanisa mashuhuri mnamo mwaka 786 BK. Kanisa hili leo hii imeshapokelewa katika orodha ya urithi wa dunia.
Tangu 1972, Aachen imekuwa moja kati ya sehemu ya Mkoa wa Kiserikali wa Cologne.
[hariri] Tazama pia
[hariri] Viungo vya Nje
| Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Aachen kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |