Nenda kwa yaliyomo

Zipu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zipu ikiunganisha pande mbili za kitambaa.

Zipu ni kifaa kinachotumika kukutanisha upande mmoja na mwingine kwenye nguo, kitambaa, begi, midoli n.k. kama tunavyoona katika picha.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Zipu ilivumbuliwa na mhandisi Gideon Sundback aliyepata hataza mnamo mwaka 1909[1] na kuboreshwa naye hadi mwaka 1917.

Zipu zilianza kutumiwa kwa kufunga viatu na baada ya miaka kadhaa ziliingia katika soko la nguo.

Mwanzoni zilitengenezwa kwa metali lakini tangu miaka ya 1950 zipu za plastiki zimeenea.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Hataza ya 4-12-1909 kwa Gideon Sundback, tovuti ya Espacenet Patent search ya European Patent Office, iliangaliwa Agosti 2019
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.