Wote Initiative for Development Empowerment

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jeremiah Wandili wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Sio Poa,Mkoani Arusha

Wote Initiative for Development Empowerment [1] (kwa kifupi WIDE) ni asasi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa na Jeremiah Wandili [2] mwaka 2018. Taasisi hii inafanya kazi zake ndani ya mipaka ya Tanzania na inapatikana katika mkoa wa Dar es salaam

Dhamira[hariri | hariri chanzo]

Kuwawezesha wanawake,watoto na vijana kufikia malengo endelevu, kupata huduma bora za afya kwa usawa, kwa njia ya elimu na kuhamasihsa haki za binadamu na kuwawezesha wananchi kichumi kwa njia shirikishi.

Dira[hariri | hariri chanzo]

Kuwa na jamii yenye uwezo wa kiuchumi,afya bora,inayojali haki za binadamu iliyoelemika kuishi katika mazingira salama.

Malengo[hariri | hariri chanzo]

Malengo ya taasisi ya WIDE ni kuiwezesha jamii kuondokana na umasikini na kuhamasisha shughuli za kiuchumi pamoja na kujenga uelewa kwa jamii katika masuala ya kijinsia, na ulinzi wa haki za wanawake na watoto. Kuhamasisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto na vijana ili kuwa taifa la watu walio elimika na wanaoweza kujitegemea. Pamoja na kuhamasisha na kujenga uelewa kwa vijana na wasichana (balehe) juu ya masuala ya Afya ya uzazi na jinsia. Kuhakikisha jamii inashiriki kikamilifu katika ulinzi wa haki za wanawake na watoto. Kuwezesha jamii kupata maji safi na salama na usafi wa mazingira.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-07-26. Iliwekwa mnamo 2021-07-26. 
  2. https://tanzania.dotrust.org/our-team/#person--jeremiah-wandili