Nenda kwa yaliyomo

Women Jazz Band

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Women Jazz Band
Women Jazz Band kazini
Women Jazz Band kazini
Maelezo ya awali
Asili yake Dar es Salaam, Tanzania
Aina ya muziki Muziki wa dansi
Miaka ya kazi 1965-

Women Jazz Band ilikuwa bendi ya muziki wa dansi kutoka Dar es Salaam, Tanzania. Bendi ilianzishwa na mnamo 1965 ikiwa na wanawake tupu, lakini baadaye ilileta wanaume kwenye upande wa kupiga vyombo.

Historia yake

[hariri | hariri chanzo]
Kijakazi Mbegu kwenye solo gitaa.
Women Jazz Band kazini
Women Jazz Band kazini
Women Jazz Band kazini

Mwaka 1965 kundi jipya la muziki la aina yake lilianzishwa Tanzania. Lilikuwa ni bendi ya akina mama watupu. Akina mama hawa, wengine wakiwa wafanya kazi wa Government Press walijichagua na kuanza kuhudhuria mafunzo ya muziki chini ya yule mwanamuziki mahiri Mzee Mayagilo aliyekuwa kiongozi wa shughuli za muziki katika Jeshi la Polisi.

Akina mama hawa wakawa chini ya kitengo cha Polisi Jazz Band, wakaanza kufanya mazoezi ya nguvu. Bendi hiyo ya akina mama ilikuwa chini ya TANU Youth League. Wakati wakianza shughuli hii walikuwa hawana ujuzi wowote wa muziki. Kutokana na jitihada waliyofanya taratibu wakaanza kufanya maonyesho yao hasa kwenye hafla za serikali na Chama tawala wakati huo.

Tarehe 31 Mei 1966 Women Jazz band iliingia katika studio za RTD na kurekodi nyimbo sita. Nazo ni:

  1. Tumsifu Mheshimiwa
  2. Leo Tunafuraha
  3. Mwalimu Kasema
  4. Women Jazz
  5. Sifa nyingi tuwasifu viongozi
  6. TANU yajenge nchi.

Washirika wakuu

[hariri | hariri chanzo]

Washiriki katika bendi hiyo walikuwa;

  1. Mary Kilima- Mwimbaji
  2. Juanita Mwegoha-Mwimbaji
  3. Siwema Salum- Mwimbaji
  4. Rukia Hassan- Mwimbaji
  5. Kijakazi Mbegu- Solo Guitar
  6. Mwanjaa Ramadhan-Bass Guitar
  7. Chano Mohammed-Rhythm Guitar
  8. Tatu Ally-Alto Sax
  9. Mina Tumaini-Tenor Sax
  10. Anna Stewart-Alto Sax
  11. Rukia Mbaraka-Tenor Sax
  12. Lea Samweli-Bongos
  13. Josephine James-Drums
  14. Zainab Mbwana-Maracass
  15. Tale Mgongo-Timing.

Mapokezi katika jamii na kuvunjika kwa kundi

[hariri | hariri chanzo]

Women Jazz ilipata umaarufu kiasi cha kuanza kufanya safari nje ya Tanzania, na kuweza kufanya maonyesho Nairobi na Mombasa, baada ya kutembelea miji kadhaa nchini Tanzania. Wakati wa matayarisho ya kwenda China kundi lilisambaratika. Kikubwa kilichosababisha hili ilikuwa ni wanamuziki kuona hawapati chochote kutokana na mapato yaliyotokana na muziki.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]