Will Voigt

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

William Voigt (kuzaliwa 18 agosti 1976) ni mwalimu wa mchezo wa mpira wa kikapu mwenye asili ya Amerika ambae kwa sasa ni mwalim mkuu wa timu ya Zamalek inayoshiriki ligi kuu huko Misri.

Akiwa kama kocha mkuu alifanikiwa kuipa ubingwa timu ya Nigeria katika mashindano ya AfroBasket ya mwaka 2015 ambapo ilishinda dhidi ya Angola katika fainali ya kufuzu katika mashindano ya 2016 ya Kiangazi ya olimpics huko Rio.[1]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Voigt amekulia katika mji wa Cobot, Vernont na kupata elimu yake katika shule ya sekomdari Caboti ambapo alicheza mpira wa kikapu na mpira wa miguu. Alipata elimu ya chuo cha kati katika chuo cha Pomona huko California, akisomea uandishi wa soka na kuhitimu na shahada ya Sayansi ya siasa.[2]

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Mama wa Voigt, Ellen Bryant Voigt alikuwa mshairi wa zamani katika Jimbo la Vermont. Voigt alioa mwaka 2009, na walitalikiana na mke wake mwaka 2018. Walipata watoto wawili, mvulana na msichana.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. BasketballWithinBorders - Training the World, One Baller at a Time (en-US). Jalada kutoka ya awali juu ya 2022-09-01. Iliwekwa mnamo 2022-09-01.
  2. "Will Voigt", Wikipedia (in English), 2022-08-20, retrieved 2022-09-04