Wilhelm Caspar Oddo
Wilhelm Caspar Oddo (alizaliwa mkoani Mbeya, Aprili 2 1987 ) ni mwana Tehama, mwandishi, mjasiriamali jamii na mfanyabiashara wa Tanzania.
Anafahamika zaidi kwa kuwa muasisi wa Chuo cha NLab Innovation Academy ambacho kabla ya kuwa chuo ilikuwa na hatamizi ya wazi kwa wanafunzi na vijana wa kike na wa kiume ili kujifunza kutengeneza mifumo ya kitehama pasipo malipo yoyote huku ikiwasaidia kuanzisha miradi yenye kufaidisha jamii na kutengeneza mazingira mazuri ya kupata nafasi za masomo ya juu na fursa mbalimbali[1]. Pia ni muasisi mwenza wa Taasisi za NLab Foundation na Apps and Girls.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa mkoani Mbeya na kukulia mkoani Njombe akiwa ni mtoto wa Pili kati ya watatu. Shule ya awali alisoma shule kadhaa ikiwemo Kilimo Primary School - Mbeya, Lugarawa Primary School - Njombe na Mtera Dam Primary school - Dodoma. Elimu ya secondary alisoma Mtera Secondary School (Ladwa) na baadaye kujiunga na Kidato cha tano na sita katika shule ya Secondary ya Biafra iliyo kuwepo Kinondoni Jijini Dar es salaam. Akiwa kidato cha Sita alipata ajali mbaya ya gari iliyobadilisha maisha yake kwa ujumla.
Alijiunga na Chuo kikuu cha Kampala International University mwaka 2007 na kuhitimu mwaka 2010 ambako alipata shahada ya sayansi ya mifumo ya taarifa (Information System).
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2010 mwishoni aliajiriwa kama Mkufunzi msaidizi huku akisoma Shahada ya utengenezaji wa Mifumo ya Compyuta (Masters of Science in Software Engineering). Mwaka 2014 mwishoni aliacha kazi rasmi na kuanzisha Hatamizi ya wazi iliyo itwa OUFLab huko Gongo la mboto jijini Dar es salaam.
Kazi za Kijamii
[hariri | hariri chanzo]- OUFLab : Mwaka 2010 mara baada ya kumaliza chuo na kuajiriwa kama Mkufunzi msaidizi katika chuo kikuu cha Kampala International University tawi la Dar Es Salaam, Wilhelm aliona tatizo kwa wanafunzi aliokuwa akiwafundisha. Wengi walitamani kuwa watengenezaji wazuri wa Mifumo na tovuti lakini changamoto ilikuwa ni ugumu wa Masomo hayo ya Kutengeneza mifumo na zaidi elimu yao ya nyuma haikuwa na msingi mzuri wenye kumfanya mwanafunzi aweze kuielewa vyema lugha ya uandishi wa Codes zenye kutengeneza mifumo hiyo. Wilhelm akaanzisha utaratibu wa kuwafundisha wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali nyumbani kwake Mzambarauni Gongo la Mboto. Na mradi huu ulioitwa OUFLab[2] ukawa ni mradi maarufu na wenye kuvutia wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali kama UDSM, IFM, KIU na vinginevyo.
- Friday Night Code: Huu ulikuwa ni mradi wa kuwakutanisha wanafunzi wa vyu mbali mbali siku ya Ijumaa jioni, wanafunzi walikuwa wakikutana Nyumbani kwa Wilhelm na kuanza kusaidiana kutengeneza mifumo usiku mzima na ifikapo asubuhi ya saa Moja wote hutawanyika na kuendelea na shughuri zao nyingine. Mmoja wa wawezeshaji katika Friday Night Code alikuwa ni Carolyne Ekyarisiima ambaye naye alikuwa ni Mkufunzi katika chuo kikuu cha Kampala International University tawi la Dar es salaam[3].
- Mafunzo ya TEHAMA kwa watoto: Hakuishia hapo, Wilhelm akaona kuna haja ya kurudi nyuma na kuanza waandaa hawa ambao wangetamani kuwa Waundaji wa mifumo ya Kitehama, na kwakuwa mtaala wa elimu ya msingi haukuwa na mafunzo hayo hivyo mwaka 2013 akaanzisha mafunzo kwa watoto, nayo yakifanyikia nyumbani kwake huko huko Gongo la Mboto.[4]
- Walimu na Tehama: Katika kuchangia juhudi za kuboresha elimu ya Tanzania Wilhelm na timu yake wakaanzisha mradi wa kufundisha Tehama kwa walimu. Mradi ulianzia NLab na baadaye kuanza zunguka mashuleni kufundisha Tehama. mafunzo yalihusisha utengenezaji wa tovuti kwa kutumia mifumo wazi ya Wordpress na Joomla, pia matumizi ya TEHAMA katika kuandaa nyenzo na matirio ya kufundishia wawapo darasani. Pia walimu wakafundishwa namna sahihi ya kutunza taarifa zao wawapo mtandaoni.
Biashara
[hariri | hariri chanzo]Wilhelm amejikita kwenye biashara zinazo husu elimu, fedha, kilimo na ufugaji.
Mijadala , Mihadhara na Mazungumzo
[hariri | hariri chanzo]Amekuwa ni mshiriki katika Mihadhara ndani na nje ya Tanzania inayo husisha elimu, kilimo, vijana, ajira, afya, mazingira na Ujinsia.
- Mkutano wa E-Learning Africa (Rwanda) mwaka 2018 - Alizungumzia (Changing the Future of Africa, One Step at a Time)[5]
Vitabu alivyoandika
[hariri | hariri chanzo]- Hatua kwa Hatua: ISBN: 978 9987 9642 1 5
- Lawama: ISBN: 978 9987 9642 1 5
- Insights: A Youth's Guide to Business Success: ISBN: 978 9987 9642 2 2
Tuzo na Teuzi
[hariri | hariri chanzo]- Private Sector Youth Inclusive Award - Ghana (2020)[6]
- AvanceMedia Most Influential Young Tanzanians (2018)[7]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-04-06. Iliwekwa mnamo 2024-04-06.
- ↑ https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/magazines/sound-living/bridging-the-digital-divide-2630106
- ↑ "Friday Night Code: Where Passion Meets Progress". East Africa Pulse. Iliwekwa mnamo 2024-04-11.
- ↑ https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/magazines/success/africa-s-education-efforts-are-shifting-in-order-to-reflect-ict-growth-2513576
- ↑ https://www.elearning-africa.com/programme/pdf/eLA2018_programme.pdf
- ↑ "Private Sector Youth Inclusive Award". Youth SDG Achievers Awards (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-11.
- ↑ "Celebrating Tanzania's Most Influential Young Entrepreneurs". East Africa Pulse. Iliwekwa mnamo 2024-04-11.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- https://www.bz-berlin.de/archiv-artikel/b-z-reporterin-suchte-eine-app-in-afrika
- https://www.oneyoungworld.com/blog/young-leaders-bringing-smile-unhappiest-countries-earth
- https://eastafricapulse.blogspot.com/2018/11/education-institution-from-tanzania.html
- http://tz.avancemedia.org/ Ilihifadhiwa 25 Machi 2017 kwenye Wayback Machine.
- https://www.indiegogo.com/projects/community-owned-computer-lab-in-tanzania#/
- https://medium.com/startupbus/buspreneur-interview-with-wilhelm-oddo-793f02961936
- https://tanzict.wordpress.com/2013/10/01/pitching-session-for-startups-congratulations-to-victronix/
- https://www.ghanaweb.com/GhanaHomePage/africa/Kuami-Eugene-Kwadwo-Sheldon-JoeBoy-among-129-young-Africans-nominated-for-2020-Africa-Youth-Awards-1134104#google_vignette
- https://pulte.nd.edu/news/notre-dame-president-rev-john-i-jenkins-c-s-c-welcomes-2018-mandela-washington-fellows-to-campus/
- https://www.modernghana.com/entertainment/65403/kuami-eugene-kwadwo-sheldon-joeboy-among-129.html
- https://www.oneyoungworld.com/news-item/calloncop-advocating-action-climate-change
- https://www.yalieastafrica.org/faq/images/The%20Leading%20Edge%20Issue%205.pdf Ilihifadhiwa 29 Julai 2023 kwenye Wayback Machine.
- https://eastafricapulse.blogspot.com/2021/03/empowering-next-generation-of-tech.html
- https://sdgachieversawards.org/speaker/private-sector-youth-inclusive-award/