Wilfredo Leòn

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Wilfredo Leòn

Wilfredo León Vimong (amezaliwa 31 Julai 1993) ni mchezaji wa kitaifa wa mpira wa wavu aliyezaliwa nchini Cuba.

Wilfredo Leòn ni mwanachama wa timu ya kitaifa ya mpira wa wavu ya Cuba (2007-2002) na mwanachama wa sasa wa timu ya kitaifa ya mpira wa wavu ya Poland na klabu ya Italia ya Sir Sicoma Conad Perugia.

Leòn alizawadiwa medali ya fedha katika Mashindano ya Dunia ya mpira wa wavu mwaka 2010, mshindi wa NORCECA (2009, 2011), bingwa wa mchezo wa mpira wa wavu wa Cuba (2009, 2010, 2011), bingwa wa mchezo wa mpira wa wavu wa Urusi (2015, 2016, 2017).

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Wilfredo Leòn alizaliwa huko Santiago de Cuba, Cuba.

Yeye ni mtoto wa Alina Vimong Boza (mchezaji wa zamani wa mpira wa wavu). Alisoma katika Escuela Nacional del Voleibol Cubano. León Vimong aliishi Poland kwa muda mfupi na mpenzi wake wa Kipolishi.

Mnamo tarehe 14 Julai 2015 alipokea uraia wa Kipolishi na alionyesha hamu yake ya kucheza katika timu ya kitaifa ya wachezaji wa mpira wa wavu wa Poland. Mnamo tarehe 24 Juni 2016 alimuoa Małgorzata (mzaliwa wa Gronkowska). Mnamo tarehe 13 Mei 2017 binti yao Natalia alizaliwa.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons