Wilfred Agbonavbare

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wilfred Agbonavbare (5 Oktoba 1966 - 27 Januari 2015) alikuwa mtaalam wa mpira wa miguu kutoka Nigeria ambaye alicheza kama kipa.

Ushiriki Katika Klabu[hariri | hariri chanzo]

Katika nchi yake, Agbonavbare alizaliwa mjini Lagos alichezea timu ya mpira ya Benki Mpya Ya Nigeria F.C Mnamo 1990,Agbonavbare alihamia Uhispania ambapo akianza kuchezea klabu ya Rayo Vallecano huko kayika ligi ya Segunda División. [1]

Ushiriki Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Agbonavbare alionekana na Timu ya Taifa Ya Nigeria chini ya miaka 20 kwenye Mashindano ya Vijana ya Dunia ya FIFA ya 1983 huko Mexico.Agbonavbare Alicheza kwa zaidi ya muongo mmoja, akichaguliwa kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika la 1994 la 1994 na Kombe la Dunia la FIFA la mwaka huo, akimuunga mkono Peter Rufai mara zote mbili.

Maisha Binafsi[hariri | hariri chanzo]

Agbonavbare aliishi katika jamii ya Madrid baada ya kustaafu kama mchezaji, akifanya kazi kama mkufunzi wa kipa. Mwisho wa Januari 2015 ilisemekana kuwa alikuwa akiugua saratani, na baadaye alipata matibabu katika Hospitali ya Universitario Príncipe de Asturias huko Alcalá de Henares.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Soler, Jaume. "El Rayo llega con la intención de puntuar", 14 April 1996. Retrieved on 28 January 2015. (Spanish) 

Viungo Vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wilfred Agbonavbare kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.