Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Makala ya wiki/Stratolaunch Roc

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

[[Picha:|100px|Stratolaunch Roc]]

Stratolaunch Roc (ing. en:Scaled Composites Stratolaunch "Roc") ni eropleni kubwa zaidi duniani tangu kuruka mara ya kwanza katika mwezi wa Aprili 2019.

Ndege hii imetengenezwa kwa kutumia ndege mbili za Boeing 747-400 ilhali injini, chumba cha rubani, magurudumu na haidroli za ndege hizi ilitumiwa. Ndege mpya ina upana mkubwa wa mabawa wa mita 117. Chini ya mabawa kuna sehemu mbili za pekee, na mzigo wa roketi utabebwa katikati chini ya mabawa. Hata kama Stratolaunch Roc ni ndege kubwa duniani kufuatana na vipimo vyake, ndege ya Antonov An-225 kutoka Ukraine inabeba mzigo ulio sawa.

Ilijengwa na kampuni ya Stratolaunch Systems kwa kusudi la kubeba roketi zinazorushwa hewani na kulenga anga-nje. Mbinu huu unapunguza gharama kwa kurusha roketi kuanzia kimo cha mita 10,500. ►Soma zaidi