Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Makala ya wiki/Goodluck Jonathan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Goodluck Jonathan

Goodluck Ebele Azikiwe Jonathan (* 20 Novemba 1957) ni rais wa Nigeria tangu Januari 2010. Awali hakuchaguliwa lakini alikabidhiwa madaraka akiwa makamu wa rais mgonjwa Umaru Yar'Adua aliyemtangulia na baada ya kifo chake aliapishwa kama rais. Katika uchaguzi wa kitaifa wa Aprili 2011 alirudishwa ofisini. Jonathan alizaliwa katika familia ya Wakristo wa kabila ya Ijaw kwenye delta ya mto Niger. Alisoma shule za msingi Otuoke na Oloibiri na tangu 1971 shule ya sekondari ya Mater Dei mjini Imiringi.

Mwaka wa 1975 hadi 1977 alifanya kazi ya idara ya ushuru na kodi. 1977 akajiandikisha kama mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Port Harcourt katika idara ya zoolojia. Baada ya kumaliza kwa digrii ya bachela alifanya kazi ya ualimu wa shule mjini Iresi. Aliendelea kusoma Chuo Kikuu hadi kupata digrii za MSc na daktari ya falsafa katika zoolojia. 1993 alikuwa makamu wa mkurugenzi wa kamati ya maendeleo ya maeneo ya kutoa mafuta Nigeria akiwajibika kwa mambo ya kuhifadhi mazingira. 1998 aliingia katika siasa. Jonathan amemwoa Patience Faka Jonathan akiwa na watoto wawili. ►Soma zaidi