Wikipedia:Makala ya wiki/Biomasi
Biomasi ni dhana muhimu katika ekolojia na ni namna ya kuangalia upande wa kimwili wa uhai duniani ni pia dhana muhimu katika maswali ya uzalishaji wa nishati hasa nishati mbadala kama biofueli.
Jumla ya miili ya viumbehai
Kimsingi biomasi ni jumla ya miili ya viumbehai vyote duniani.
Kiasi kikubwa ni mimea lakini miili ya wanyama au planktoni huhesabiwa pia. Vilevile wanyama na mimea iliyokufa, kukauka, kuoza na kadhalika ni sehemu ya biomasi. Sehemu zao hutumiwa na viumbehai vingine kama lishe la kujenga biomasi mpya.
Msingi wa biomasi ni mchakato wa usanisinuru katika mimea ambako nishati ya jua inawezesha mmea kujenga mwili wake kwa kuunganisha kemikali asilia kutoka mazingira yake.
Fueli kisukuu kama mafuta ya petroli au makaa mawe ziliundwa pia kutokana na biomasi lakini huhesabiwa mle kwa sababu zimepitia mabadiliko na kufikia hali isiyotumiwa tena kama lishe ya viumbehai.
Matumizi ya biomasi
Biomasi inatunza nani yake pia kiasi kikubwa cha gesi ya dioksidi kabonia ambayo menginevyo ni gesi inayowezakuchangia kwa kupanda kwa halijoto duniani na ikishikwa ndani ya biomasi kasi ya kupanda kwa halijoti inacheleweshwa.
Yaliyomo
- Jumla ya miili ya viumbehai
- Matumizi ya biomasi
- Biomasi kama chanzo cha nishati mbadala
- Viungo vya Nje
- Marejeo