Wikipedia:Kufuta makala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yafuatayo bado ni pendekezo linalohitaji kuangaliwa na kukubaliwa

Kufuta makala ni kazi ya wakabidhi. Kila mtu anaweza kupendekeza makala kwa ufutaji na kushiriki katika majadiliano, lakini wakabidhi pekee wana mamlaka ya kufuta kurasa, jamii, na picha. Wakati mwingine, kurasa zinaweza kufutwa mara moja kufuatana na azimio la mkabidhi mmoja tu.

Kwa kawaida tunaacha kufuata utaratibu kwamba mmoja anapendekeza makala ifutwe, kupekeleka jina kwenye ukurasa wa Wikipedia:Makala kwa ufutaji na hapa inaweza kujadiliwa.Mwanzoni mwa makala tunataka kufuta tuweke msimbo wa {{futa}}. Baada ya siku kadhaa mkabidi mwingine anaamua kuifuta au kuiacha, kwa kawaida baada ya maboresho.

Mara nyingi ni afadhali kuboresha makala kuliko kuifuta. Mara nyingi inaweza kusaidia pia kubadilisha makala mbaya kuwa makala ye kielekezo (Redirect) kuliko kuifuta kabisa maana kutunza jina itamsaidia msomaji kufikia kwenye habari yenye maana.

Kama tunaamua kufuta makala ni vema kuangalia kwanza "Viungo viungavyo ukurasa huu" katika menyu ya "vifaa" na kuondoa viungo vyote kwa ukurasa tutakayofuta.

Kama ukurasa umefutwa kimakosa unaweza kurudishwa na mkabidhi yeyote kupitia Maalum:Usifute (restore).

Sababu za kufuta haraka

  1. Maudhui yote ni upuuzi dhahiri. Upuuzi ni pamoja na maudhui ambayo hayana maana. Hata hivyo, hii si pamoja na staili mbaya, lugha mbaya, uharibifu, habari bandia.
  2. Kurasa zinazoaandikwa kwa lugha isiyo Kiswahili (mfano kuunda makala kwa kutumia Kiingereza ; tufute, isipokuwa inaruhusiwa kwenye ukurasa wa mtumiaji)
  3. Ukurasa wa majaribio, kama vile "Je! Ninaweza kuunda ukurasa hapa?".
  4. Marudio ya maudhui ambayo yamefutwa tayari. (Mfano mtu ameleta makala juu yake mwenyewe, iligunduliwa na kufutwa, anarudia kuleta makala akibadilisha jina kidogo lakini ni yeye yule)
  5. Kusafisha tovuti: mfano kama kuna makala maradufu kuhusu jambo lilelile, habari zimeshaunganishwa upande mmoja. Sasa tunapaswa kufuta makala nyingine au afadhali kutumia nafasi yake kama Kielekezo (#REDIRECT [[ukurasa lengwa]]).
  6. Mwandishi anaomba ufutaji: Ukurasa wowote ambao mwandishi wa asili anataka ufutwe, unaweza kufutwa haraka, mradi tu wengine hawajachangia katika matini yake. Ikiwa mwandishi mwenyewe anafuta maandishi, hii inaweza kumaanisha kuwa anataka ifutwe.
  7. Kurasa zinazotegemea kurasa zilizofutwa au ambazo hazipo zinaweza kufutwa, isipokuwa kama zina mjadala juu ya ufutaji ambao hauwezi kupatikana mahali pengine popote.
  8. Kurasa za shambulio au matusi. Kurasa ambazo ziliundwa tu kumtukana mtu au kitu (kama vile "John ni bubu"). Hii ni pamoja na nakala juu ya mtu aliye hai ambaye hutukana tu na hana vyanzo, na ambapo hakuna toleo la NPOV katika historia ya kuhariri kurudi.
  9. Matangazo dhahiri: Kurasa ambazo ziliundwa tu kusema mambo mazuri juu ya kampuni, bidhaa, kikundi au huduma na ambayo itahitaji kuandikwa tena ili waweze kufaa kwenye kamusi elezo. Hata hivyo makala kuhusu kampuni, bidhaa, kikundi au huduma vinavyotimiza matakwa ya Wikipedia:Umaarufu katika jamii kama mada yake itabaki.
  10. Kurasa zinazovunja sheria ya hakimiliki kama ukurasa ambao:
    • Umenakiliwa kutoka kwa tovuti nyingine ambayo haina leseni ambayo inaweza kutumika na Wikipedia.
    • Hauna yaliyomo kwenye historia ya ukurasa ambayo inafaa kuokolewa.
    • Umeongezwa na mtu ambaye haambii ikiwa amepata ruhusa ya kufanya hivyo au la, au ikiwa dai lao lina nafasi kubwa ya kutokuwa kweli. Hii ni pamoja na kunakili kutoka kwa Wikipedias nyingine bila uainishaji sahihi.
Tunapofuta makala au kuipeleka kwenye ukurasa wa ufutaji, tunamwarifu mtungaji pia. Mara nyingi ni mchangiaji anayehitaji kujifunza.

Tazama pia