Wikipedia:Kielekezo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alama ya Kielekezo katika menyu ya "Kuhariri chanzo"

Kielekezo au elekezo ni ukurasa wa Wikipedia inayompeleka mtumiaji kwenda ukurasa mwingine.

Tunatumia vielekezo kama msaada wa kumfikisha mtumiaji katika habari fulani. Kwa mfano kama mtu, jambo au mahali wanajulikana kwa majina mawili tofauti, tunatumia jina ambalo ni kawaida zaidi (au rasmi) kwa makala yenyewe na jina mbadala kwa ukurasa wa kielekezo.

Katika menyu ya "Hariri chanzo" kuna alama inayoonyeshwa. Inafungua dirisha tunapoweka jina la ukurasa tunapoelekeza. Badala yake tunaweza kuandika pia msimbo #REDIRECT [[xxxx]] (xxxx ni jina la makala) ikiwa ni matini pekee kwenye ukurasa wa kielekezo.