Watengwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Watengwa ni kundi la muziki kutoka Arusha, Tanzania.

Kundi hili lilianzishwa mnamo mwaka 1999 katika eneo linaloitwa Kijenge Juu. Kundi hili ni maarufu kwa aina ya muziki wao wa Hip Hop, Ragga, Reggae, Afrobeat, n.k. nchini Tanzania na pia inasemekana ni kundi linalobeba wasanii wengi kuliko makundi mengi ya hip hop Afrika.

Kundi hili linafanya muziki unaogusa maisha na harakati za wanajamii na wanamuziki pia. Watengwa ni JCB Makalla, Chindo aka Umbwa Mzee, Donnie, Alwatan Kwelle, Daz Naledge, Chabba, Ghost B, Kekuu, D Wee, Lau, Mathieu, Ghetto Queen,frost, Chaca Na Nduguzee, Yuzzo Rubama na wengine wengi kwa kada zao mbalimbali.

Iliandikwa[hariri | hariri chanzo]

Iliandikwa ilikuwa albamu ya kwanza ya watengwa iliyosikika sana kwa washabiki, albamu hii ilitengenezwa chini ya studio za Watengwa records ikiwa na wimbo maarufu 'Nawaza' ambao ulimuhusisha Chindo Man. Wimbo wa JCB, 'Nimefurahishwa' nao pia ulifanya vizuri kwenye redio na kuwatambulisha JCB na Chindo Man kama vinara wa kundi hili. Nyimbo nyingine zilikuwa ni 'Back 2 The Suwa', Taarifa Ya Habari JCB akimshirikisha Chaca, Ukiskia Paa Vol Part 1, Iliandikwa na nyinginezo,Jcb ni moja kati ya wasanii wanaofahamika zaidi kwa kua na misimamo yake

Full ile Laana[hariri | hariri chanzo]

Hii ni albamu ya pili kutoka katika kundi la Watengwa. Albamu hii pia ilikamilishwa chini ya Studio za Watengwa. Full ile Laana ilifanya vizuri zaidi kuliko albamu iliyotangulia na kufanya Watengwa wajulikane zaidi na zaidi. Ndani ya albamu hii kulikuwa na nyimbo kama 'Sio Lazima', 'Mwafrika','Hatujaja Kujaribu' na Full ile Laana' ambazo zilifanya vizuri ndani ya Arusha na kupelekea kundi hili kuwa kundi maarufu kuliko yote Arusha.

Pigo Takatifu[hariri | hariri chanzo]

Hii ni albamu ya tatu kutoka katika kundi hili. Albamu hii ilibeba nyimbo kama 'Jicho la Tatu', 'Pigo Takatifu', na Taxi.

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Watengwa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.