Nenda kwa yaliyomo

Wahuni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuhusu makabila kutoka Asia yaiyoamia Ulaya katika karne za 4 na 5, angalia Wahunni

Wahuni (kutoka neno la Kiarabu) ni watu wasio na maadili mema. Mfano ni kikundi cha vijana waishio mitaani ambao wengi hawana kazi. Pengine hupendelea kukaa vijiweni wakishiriki matumizi ya vilevi au mihadarati. Hao huweza kuanzisha fujo kama vile ugomvi, wizi wa mali za watu n.k.

Wahuni hawana tofauti na wapumbavu kwa sababu huamini ya kwao bila ya kujifunza na kupokea mawazo mbadala.

Katika Tanzania na nchi nyingine nyingi wahuni hupatikana hasa mijini.

Saikolojia na sosholojia zinachunguza sababu za uhuni ili kupendekeza la kufanya.

Kati ya sababu hizo kuna:

  • Ugumu wa maisha
  • Ukosefu wa maadili mema katika jamii
  • Mabadiliko ya teknolojia na maendeleo ya jamii husika
  • Ukosefu wa lishe bora na magonjwa husababisha kutokea kwa vizalia wengi na wenye malezi ya mlengo wa kushoto