Wahacha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wahacha ni kabila dogo sana la watu wanaotumia lugha ya Kihacha, lugha inayozungumzwa nchini Tanzania mkoa wa Mara, hasa katika Wilaya ya Rorya.

Wahacha ni jamii yenye umoja sana. Asili yao ni kutokea maeneo ya Kenya.

Wahacha wanaendana sana na Wasweta kwa mila na utamaduni. Wanaamini sana katika ukeketaji. Jamii hii haitumii nyama aina ya paa kutokana na matukio ya kihistoria katika enzi za uwindaji hapo zamani.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wahacha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.