Waazeri
Mandhari
Waazeri (pia: Waazerbaijani, Waturuki wa Azerbaijan) ni watu wanaoongea lugha ya Kiazeri, wakazi hasa wa kaskazini-magharibi mwa Iran na nchi ya Azerbaijan.
Idadi yao hukadiriwa kuwa kati ya milioni 25 - 30; wengi wanaishi Iran (milioni 15) na Azarbaijan (milioni 9). Wachache wako pia Uturuki, Georgia na Armenia. Karibu wote ni Waislamu wa dhehebu la Shia.
Asili yao ni mchanganyiko wa mataifa na makabila mbalimbali. Watu wa maeneo ya Azerbaijan walikuwa wameanza kutumia Kiajemi kabla ya uvamizi wa Waarabu. Tangu karne ya 11 makabila ya Kituruki walipita hapa katika uhamisho wao kutoka Asia ya Kati kuelekea magharibi, wengi walibaki. Polepole wakazi walibadilisha tena lugha hadi Kiturki cha wageni kimekuwa lugha ya wananchi.