Vito Mannone

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vito Mannone
Maelezo binafsi
Jina kamili Vito Mannone
Tarehe ya kuzaliwa 2 Machi 1988
Mahala pa kuzaliwa    Desio, Italia
Urefu 1.91m
Nafasi anayochezea Golikipa
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Arsenal
Namba 24
Klabu za vijana
2003–2005
2005-2006
Atalanta B.C.
Arsenal FC
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2006
2006-
Barnsley FC
Arsenal
Timu ya taifa
2009- Italia

* Magoli alioshinda

Vito Mannone (alizaliwa 2 Machi 1988) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Italia ambaye anacheza katika nafasi ya golikipa katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Wasifu wa Klabu[hariri | hariri chanzo]

Wasifu wa hapo awali[hariri | hariri chanzo]

Mannone alitia saini mkataba na Arsene Wenger katika mwaka wa 2005, akiungana na Arsenal kutoka timu ya Atalanta katika mkataba wa miaka tatu na kulipa ada ya £ 350.000 ya fidia, kwa kuwa hakuwa ameunda mkataba na timu hiyo ya Uitalia. Yeye alicheza kwa mara ya kwanza katika timu ya Arsenal katika mechi ya kirafiki dhidi ya Barnet mnamo 16 Julai 2005.Arsenal ilishinda mechi hiyo 4-1.

Muda wa mkopo akiwa Barnsley[hariri | hariri chanzo]

18 Agosti 2006, Mannone alihamia timu ya Barnsley kwa muda wa miezi mitatu katika mpango wa mkopo, alitarajiwa ,kung'ang'ania nafasi ya golikipa na Nick Colgan. Mannone ,alipokuwa Barnsley, hakufurahia - katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Preston North End mnamo 22 Septemba 2006, aliingia mechi kama mchezaji mbadala baada ya Colgan kuonyeshwa kadi nyekundu. Alikuwa na bahati mbaya alipofanya Preston kushinda kwa kupiga mpira na ukagonga kichwa cha Patrick Agyemang na kuwa bao. Katika mechi iliyofuata dhidi ya Luton Town, alianza katika mechi hiyo badala ya Colgan,akafanya kosa na akafungwa na Ahmet Brkovic,wakashindwa.

Kurudi Arsenal[hariri | hariri chanzo]

Aliumia katika goti lake,hili jeraha likakatiza muda wake wa mkopo na akarudi Arsenal kwa matibabu. Kulikuwa na uvumi kuwa alikuwa anaenda Ligi Kuu ya Scotland kucheza katika timu ya Inverness CT hapo Januari 2007. Mpango huo haukufaulu walipokosa kumthibitishia kuwa atacheza katika timu ya kwanza. Alihusishwa na mpango wa mkopo kuenda kucheza katika timu ya Gretna katika Ligi Kuu ya Scotland katika mwaka wa 2007.Mpango huo haukufaulu pia.

Mannone alicheza mara kwa mara chini ya Lukasz Fabianski katika kampeni ya Arsenal katika Shindano la Kombe la League ya mwaka wa 2007-08. Hata hivyo,hakucheza hata mechi moja katika mechi tano ya klabu hiyo katika shindano hilo.Walitolewa kutoka kwenye shindano na timu ya Tottenham Hotspurs. Mnamo 19 Desemba 2007, Arsenal ilitangaza kuwa Mannone alikuwa ametiaa saini mkataba mpya wa muda mrefu. [12] Hapo 19 Aprili 2008, yeye alikuwa mmoja wa wachezaji waliochaguliwa katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Reading katika Uwanja wa Emirates lakini hakucheza mechi hiyo.Jens Lehmann ndiye aliyelinda lango.

Kufuatia kuondoka kwa Jens Lehmann katika mwaka wa 2008, Mannone akawa chaguo la tatu katika nafasi ya golikipa , akifuata MAnuel Almunia na Lukasz Fabianski. Mannone alibadilisha nambari yake ya jezi kutoka #40 kuwa #24 katika mwanzo wa msimu wa 2008-09 baada ya aliyekuwa #24 ,Almunia, kupewa jezi #1. 19 Julai 2008, yeye alicheza nusu ya pili ya mechi ya kabla ya msimu ya kirafiki dhidi ya Barnet huko Underhill huku akikosa kufungwa bao. Kabla ya msimu kuanza , alicheza katika mechi 4 katika timu ya kwnza ya Arsenal akiingia kama mchezaji mbadala wakati wote katika nusu ya mechi.

Alicheza mechi yake ya kwanza muhimu akiwa Arsenal katika mechi ya mwisho ya msimu wa 2008-09,dhidi ya Stoke City mnamo 24 Mei 2009.~ Arsenal ilishinda mechi hiyo 4-1. [14]

Msimu wa 2009/10[hariri | hariri chanzo]

Manuel Almunia na Lukasz Fabianski walipokuwa wameumia, Vito alicheza katika mechi yake ya kwanza katika Shindano la Mabingwa la UEFA dhidi ya Standard Liege, mechi ya Arsenal ya kwanza katika mkondo wa vikundi mnamo 16 Septemba 2009. Mechi hiyo ilianza vibaya sana,huku akifungwa mabao mawili katika dakika tano za kwanza,bao moja likiwa mkwaju mkali wa Mangala ambao ulimshinda Vito na kuingia.Bao la pili lilikuwa mkwaju wa penalti baada ya Jovanovic kutendewa maovu na William Gallas. Hata hivyo, Arsenal ilifanya juhudi na kushinda mechi hiyo 3-2 kwa mabao ya Nicklas Bendtner,Thomas Vermaleen na Eduardo da SIlva.

Manuel Almunia alpokuwa bado nje, Mannone alicheza katika mechi yake ya pili ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Wigan mnamo 19 Septemba 2009. Mannone hakufungwa bao lolote katika mechi hiyo walioshinda 4-0. Mannone pia hakufungwa bao lolote katika mechi dhidi ya Fulham katika uga wa Craven Cottage mnamo 26 Septemba. Katika mechi hiyo,aliokoa Arsenal kwa kulinda lango kwa umahiri mkubwa na akashinda tuzo la Mchezaji Bora Katika Mechi,Arsenal walishinda 1-0. Mannone alisema kuwa mechi hiyo ndiyo iliyokuwa bora kabisa katika kazi yake ya kuwa golikipa. Hakufungwa bao lolote katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Olympiakos katika Shindano la Mabingwa la UEFA mnamo 29 Septemba.

Tarehe 17 Oktoba 2009,Mannone aliteuliwa kama golikipa katika timu ya kwanza badala ya yule wa hapo awali,Manuel Almunia, aliyekuwa akiugua maradhi fulani.Hii ilionekana kuwa kuonyesha imani katika Mannone na kuuliza maswali juu ya nafasi ya golikipa ilikuwa ya nani.

Wasifu wa Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 13 Novemba 2009, Vito alicheza kwa mara ya kwanza timu ya Uitalia ya vijana walio chini ya umri wa miaka 21 katka mechi dhidi ya Hungaria.

Takwimu ya Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Klabu Msimu Ligi Kombe Uropa Jumla
Mechi alizocheza Mabao Usaidizi katika kufunga bao. Mechi alizocheza Mabao Usaidizi katika kufunga bao. Mechi alizocheza Mabao Usaidizi katika kufunga bao. Mechi alizocheza Mabao Usaidizi katika kufunga bao.
Arsenal 2005–06 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0
Barnsley 2006–07 2 0 0 2 0 0 0 0 0 4 0 0
Arsenal 2007–08 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0
2008–09 1 0 0 0 0 0 0 0 0 1 0 0
2009–10 5 0 0 0 0 0 3 0 0 8 0 0
Jumla 8 0 0 2 0 0 3 0 0 13 0 0

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Vito Mannone Bio, BBC Sport,
  2. Squad Profiles, Archived 27 Februari 2010 at the Wayback Machine. Espn,
  3. "Tykes loan for Gunners goalkeeper". BBC Sport. .
  4. "Preston North End 1 Barnsley 0 Archived 8 Oktoba 2006 at the Wayback Machine.: Mannone misfortune gifts Preston the points". The Independent.
  5. "No. 1 snag hits Gretna". icScotland.
  6. "Arsenal 4-1 Stoke". BBC. 24 Mei 2009.
  7. http://news.bbc.co.uk/sport1/hi/football/eng_prem/8270588.stm

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]