Vitabu vya Unabii wa Baadaye
Mandhari
Vitabu vya Unabii wa Baadaye ni vitabu 4 vya Thanak (Biblia ya Kiebrania) ambavyo katika Biblia ya Kikristo vimegawiwa na kuhesabiwa 15.
Ni kwamba Waisraeli waligawanya vitabu vyao vya unabii katika sehemu mbili zilizoitwa Vitabu vya Unabii wa Awali (Kitabu cha Yoshua, Waamuzi, Samweli na Vitabu vya Wafalme), na Vitabu vya Unabii wa Baadaye (kitabu cha Isaya, kitabu cha Yeremia, kitabu cha Ezekieli na vitabu 12 vya manabii wadogo).
Katika vitabu vya Unabii wa Awali, Mungu alidhihirisha makusudi yake kwa njia ya historia ya Waisraeli, na kwa kweli mataifa yote yalikuwa chini ya utawala wake mkuu.
Katika vitabu vya Unabii wa Baadaye, Mungu alidhihirisha makusudi yake zaidi kwa njia ya maneno ya wasemaji wake.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vitabu vya Unabii wa Baadaye kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |