Nenda kwa yaliyomo

Village Voice Media

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Takwimu kuonyesha ukuaji wa tovuti za magazeti mbalimbali ya Village Voice Media

Village Voice Media ni shirika la binafsi linalomiliki Village Voice, gazeti zee kabisa na kubwa kabisa Marekani la kila wiki (lililoanzishwa katika mwaka wa 1955). Vilevile, magazeti ya LA Weekly, OC Weekly katika Orange County, California, Seattle Weekly, City Pages katika Minneapolis-St. Paul, Nashville Scene, Dallas Observer, Westword katika Denver, New Times Broward-katika Palm Beach, Houston Press, The Pitch katika Kansas City, Miami New Times, Phoenix New Times, SF Weekly mjini San Francisco, Riverfront Times mjini St. Louis, na backpage.com,tovuti ya matangazo.Shirika la New Times Media lilikuwa la kuchapisha magazeti ya kila wiki.

Hapo awali kampuni hii ilikuwa ikiitwa New Times Media. Tarehe 24 Oktoba 2005, New Times Media ilitangaza mpango wa kununua Village Voice Media,walipofanya hivyo waliunda mnyororo wa magazeti 17 wa kuchapishwa kila wiki nchini Marekani. Baada ya kukamilika kwa mpango huo, New Times ilianza kulitumia jina la Village Voice Media.

Katika mwaka wa 2002, Village Voice Media ya hapo awali iliingia mkataba usiokuwa wa kushindana na New Times Media, wakati huo New Times Media ulikuwa pia jumba la uchapishaji magazeti ya kila wiki. Mkataba wao ulikuwa wa kutochapisha magazeti ya New Times LA(jarida la New Times Media) na Cleveland Free Times (jarida la Village Voice Media) ili zisiwe na magazeti mawili yanayoshindana katika mji mmoja. Mkataba huu na kufutiliwa mbali kwa magazeti hayo mawili ulisababisha upelelezi na Idara ya Haki ya Marekani. Matokeo ya uchunguzi yalisababisha malipo, ambapo kampuni zote mbili zilihitaji kuuza mali na magazeti hayo mawili kwa washindani wao wowote.

Mnamo Oktoba 2007, Michael Lacey, mhariri mkuu na Jim Larkin ,mkurugenzi mkuu wa Village Voice Media, walishikwa na polisi wakiwa Phoenix,Arizona kwa mashtaka ya kuwa jarida moja la Phoenix New Times lilikuwa limechapisha habari ya siri kuhusu watu wa juri. Mwendesha mashtaka maalum alifanya uchunguzi wa kesi kubwa iliyokuwa baina ya gazeti hilo na mkuu wa polisi wa kata la Maricopa,Joe Arpaio, ambapo walichapisha anwani ya Joe Arpaio,hili ni kosa la uhalifu katika sheria ya Arizona.

Angalia Pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Savannah Blackwell, "New Times nailed" Archived 2014-01-11 at Archive.today, sfbg.com, 29 Januari 2003.
  2. David Carr, "Media Executives Arrested in Phoenix", The New York Times, 19 Oktoba 2007.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]