OC Weekly

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Aina ya gazeti:
Gazeti la kila wiki
Mmiliki:
Village Voice Media
Mhariri:
Ted Kissell
Makao makuu:
2975 Red Hill Ave.Suite 150 Costa Mesa, CA 92626 Marekani Marekani
Nakala zinazosambazwa
77,982
Tovuti Rasmi:
http://www.ocweekly.com

Historia[hariri | hariri chanzo]

OC Weekly, gazeti dada kwa yale ya LA Weekly na The Village Voice. Hili ni jarida lenye ni bure na linalochapishwa kila wiki na kusambazwa hulo Orange County,California na pia Long Beach. Makala yake ya kisiasa ni ya kimaendeleo kwa jumla.

Jarida hili linaangazia sana wanasiasa wa eneo hilo kutoka vyama vyote viwili,hasa wale wa Republican waliokuwa wengi zaidi huko. Gazeti hli hukosoa wanasiasa wanafiki katika eneo hilo na huendeleza pia makala yenye mafanikio inayojulikana kama Navel Gazing.

Miongoni mwa makala mengi maarufu, ni yale yanayoitwa "¡Ask a Mexican!" ikimaanisha: Muulize mwananchi wa Mexico! yaliyoandikwa na Gustavo Arellano, makala yao ya chakula, na pia makala ,yaliyoshinda tuzo, ya upelelezi wa R. Scott Moxley, Nick Schou na Matt Coker. Makala ya wiki ya OC Weekly yamesababisha kushikwa kwa waasi na FBI, imesababisha ,pia, kufunguliwa kwa mashtaka kwa meya wawili wa Huntington Beach, kuachiliwa kwa watu wasiokuwa na hatia kutoka gerezani na likaonyesha wazi ushirikiano kati ya mkuu wa polisi na mhalifu. Mwanzoni mwa mwaka wa 2009, mkuu huyo wa polisi alihukumiwa miezi 66 katika gereza la jimbo hilo. Kazi nyingine maarufuni uzinduzi wa kashfa ya ngono katika Kanisa ya Kikatholiki, kufichua barabara za Orange County zilizotoza ada ya juu na vikundi vya chuki katika kata hilo. Makala yao hutajwa sana katika Ripoti ya Upelelezi ya Kituo cha Sheria kuhusu Umaskini. Katika mwaka wa 2009, mwanachama mashuhuri wa Republican wa eneo la California, ambaye alikuwa pia naibu mwenyekiti wa kamati ingine yenye nguvu sana katika utawala wa eneo hilo, alijiuzulu baada ya saa chache ya OC Weekly kufichua uhusiano wake wa kimapenzi na afisa wa kampuni kubwa ya California.

Jarida hili hupatikana kwa urahisi katika mikahawa,maduka ya vitabu, maduka ya mavazi,maduka mbalimbali na kokote mitaani huko.

OC Weekly hufurahia orodha zake za sanaa na burudani katika kata la Orange na pia Los Angeles, huku wakishindana na Orange County Register na Los Angeles Times.

Kwa kuwa OC Weekly ni gazeti la bure, ni lazima litegemee mapato ya matangazo yanayochapishwa ndani yake. Bali na matangazo ya maduka ya mavazi,mikahawa na vilabu vya usiku kuna matangazo ya upasuaji,huduma mbalimbali na vilabu mbalimbali.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "OC Weekly". Association of Alternative Newsweeklies

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]