Viktor Kovalenko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Huyu ni Viktor Kovalenko

Viktor Kovalenko (alizaliwa 14 Februari 1996) ni mchezaji wa soka wa Kiukreni ambaye anacheza kama kiungo wa klabu ya FC Shakhtar Donetsk katika Ligi Kuu ya Ukraina na timu ya taifa ya Ukraina.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Kovalenko ni moja ya zao la timu ya vijana ya klabu ya FC Shakhtar Donetsk.Alicheza kwa mara ya kwanza katika Ligi ya kuu ya Ukraine katika klabu hiyo ya Shakhtar kwenye mechi dhidi ya FC Vorskla Poltava mnamo 28 Februari 2015.

Mnamo 9 Mei 2015, alitoa mchango wake wa kwanza katika timu yake kwa mara ya kwanza wakati akiifungia timu yake magoli mawili goli la tano na la sita katika ushindi wa 7-1 dhidi ya FC Hoverla Uzhhorod.

Kazi ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Kovalenko aliitwa na timu ya taifa ya Ukraine kucheza kwenye Kombe la Dunia la FIFA chini ya miaka 20 huko New Zealand. Alifunga mabao mawili katika ushindi wa magoli 6-0 dhidi ya Myanmar na kushinda "hat-trick" yaani magoli matatu dhidi ya Merika kupata ushindi wa magoli 3-0 kwenye Uwanja wa Bandari ya North huko Auckland, wakati timu hiyo ilifikia hatua ya 16 bora. Alishinda tuzo ya "Golden Boot" yaani mfungaji bora wa Kombe la Dunia la FIFA chini ya miaka 20 akiwa na magoli 5.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Viktor Kovalenko kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.