Victor Hipolito Martínez

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Naibu Rais wa 29 wa Argentina
Muda alipokuwa ofisini
10 Desemba 1983 – 8 Julai 1989
Rais wake: Raúl Alfonsín
Kabla yake: María Estela Martínez de Perón
Baada yake: Eduardo Duhalde
Alizaliwa: 1924
Katika eneo la Córdoba, Argentina

Historia[hariri | hariri chanzo]

Víctor Hipólito Martínez (alizaliwa katika mwaka wa 1924) ni mwanasheria na mwanasiasa wa Argentina. Anajulikana zaidi kwa jukumu lake kama Naibu wa Rais wakati wa uongozi wa Raúl Alfonsín wa miaka ya 1983-1989.

Maisha na nyakati[hariri | hariri chanzo]

Martínez alizaliwa na kulelewa jijini Córdoba ,Argentina. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Cordoba na akafuzu na digrii katika somo la sheria katika mwaka wa 1948.Ilpofika mwaka wa 1955,alihusika katika mkutano wa Chuo Kikuu cha Southern Methodist kuhusu sera ya kawi ya fossili. Alianza kufundisha sheria ya ardhi katika mwaka wa 1956 na kupata tuzo ya juris doctor katika mwaka wa 1957. Alikuwa mhusika sana katika muungano wa Radical Civic Union (UCR),Martineza aliingia siasa na kuteuliwa kuingia Seneti ya Majimbo katika mwaka wa 1962. Alichaguliwa kama Meya wa Cordoba hasa katika mwaka wa 1963 na akabaki katika cheo hicho hadi mapinduzi ya serikali yalipofanyika na kumtoa Rais Arturo Illia(mwenzake katika UCR) katika mwaka wa 1966.

Martínez alirudi uwanja wa wasomi na akawa mhariri wa Los Principios, gazeti la eneo hilo,katika miaka ya 1970 hadi 1972. Katika uchaguzi wa mwaka wa 1973,aligombea kiti cha Gavana wa Jimbo la Cordoba na akashinda. Aliendelea kufunza katika chuo kikuu,akifanya kazi katika makamati ya serikali katika madaraja ya mitaa,majimbo na kitaifa kuhusu sheria za ardhi. Alianzisha Muungano wa Argentina wa Maliasili,Sheria na Usimamizi na akapewa cheo cha Mkuu wa Idara ya Sheria ya Ardhi katika Chuo Kikuu cha Cordoba katika mwaka wa 1979.

Kufuatia miaka saba ya uongozi wa kijeshi ulipofeli, uchaguzi ukaaandaliwa katika mwezi wa Oktoba 1983. UCR,iliyoandaa mikutano yao Julai mwaka huo,ilimchagua mwanasheria wa haki za kibinadamu,Raul Alfonsin kugombea urais na Martinez kama naibu wake. Martinez aliyekuwa mhafidhina alikuwa amechaguliwa ili kumsaidia Raul kushinda. Kufuatia wiki za kupigia kura, na kutokuwa na mshindi wazi baina ya Chama cha Justicialista na UCR,UCR ilishinda hatimaye na asilimia ya 12.Martinez akawa Naibu wa Rais.

Aliapishwa hapo 10 Desemba, jukumu lake Martinez kama Rais wa Seneti ya Argentina likawa muhimu sana kwa kuwa Justicialista walikuwa na Seneti 21 na UCR walikuwa na 18. Hata hivyo,alishindwa kuzuia kushindwa kwa Sheria ya Leba ya Alfonsin wa 1984 ama ile ya kusongezwa kwa jiji kuu hadi Viedna(masuala muhimu kwa Rais). Martínez alifanya ziara za udiplomasia mbalimbali za nje ya nchi akiwa Naibu wa Rais.Alipewa hadhi ya Mzalendo Mteule wa California na Gavana George Deukmejian katika mwaka wa 1985 na Mwanachama Mteule wa Muungano wa Inter American Bar Association katika mwaka wa 1986. Hatimaye, hata hivyo, mgogoro mkali wa pesa na maandamano ya ghafla yalimlazimisha Alfonsin kuharakishakwa miezi mitano uzinduzi wa rais mpya,Carlos Menem. Martinez alijiuzulu katika mwezi wa Juni (ilianza tangu 8 Julai Menem alipochukua uongozi).

Alirudi kufanya kazi katika sheria zinazohusu ardhi baadaye na akashinda tuzo mbalimbali kama Msalaba wa Taji la Uitalia. Martinez alipewa kiti cha heshima katika ibada ya kumbukumbu ya Rais Raul Alfonsin,aliyekufa 31 Machi 2009. Mpwa wake,Pilar Nores Bodereau, aliolewa na Alan Garcia ,Rais wa Peru, tangu mwaka wa 1978.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ Academia Nacional de Derecho y Ciencias Sociales: Víctor Matínez Archived Machi 3, 2016 at the Wayback Machine. Lugha ya Kihispania
  2. ^ Todo Argentina: 1983 Lugha ya Kihispania
  3. ^ Todo Argentina: 1989 Lugha ya Kihispania
  4. ^ La Hora de Juan Cruz: Entrevista a Víctor Martínez Lugha ya Kihispania