Nenda kwa yaliyomo

Victoire Ingabire Umuhoza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Victoire Ingabire Umuhoza
Maelezo zaidi Victoire Ingabire Umuhoza - Kiongozi wa upinzani wa Rwanda
Maelezo zaidi Victoire Ingabire Umuhoza - Kiongozi wa upinzani wa Rwanda
mwenyekiti wa Unified Democratic Forces
Chama UDF
Kazi Mwanasiasa


Victoire Ingabire Umuhoza (alizaliwa tarehe 3 Oktoba 1968) ni mwanasiasa wa Rwanda ambaye alihudumu kama mwenyekiti wa Unified Democratic Forces kutoka mwaka 2006 hadi 2019. Kama mtetezi wa demokrasia na mkosoaji wa Rais Paul Kagame, alikuwa mgombea wa UDF katika uchaguzi wa urais wa Rwanda wa mwaka 2010, lakini hatimaye alikamatwa na kuhukumiwa kifungo gerezani.[1] Akiwa mgombea wa Tuzo ya Sakharov, alitumikia miaka 8 kati ya kifungo cha miaka 15 gerezani katika Gereza Kuu la Kigali kwa mashtaka ya ugaidi na kutishia usalama wa taifa[2][3]. Kwa sasa anaongoza chama cha Development And Liberty For All, kikiwa na lengo la kampeni kwa ajili ya nafasi zaidi kisiasa na kwa ajili ya maendeleo.[4][5]

  1. "Rwanda terror charge for opposition's Victoire Ingabire", BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2010-10-25, iliwekwa mnamo 2024-04-30
  2. "Rwanda: Setting the Scene for Elections: Two Decades of Silencing Dissent in Rwanda". Amnesty International (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
  3. therwd (2018-09-17). "How Kagame Deceived The World That He Freed Victoire Ingabire Umuhoza". Therwandan (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
  4. https://dalfa.org/en/wp-content/uploads/2019/11/PRESS-RELEASE-DALFA-UMURINZI-ENGLISH.pdf
  5. https://dalfa.org/en/wp-content/uploads/2019/11/PRESS-RELEASE-DALFA-UMURINZI-ENGLISH.pdf
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Victoire Ingabire Umuhoza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.