Uwanja wa michezo wa Khomasdal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uwanja wa michezo wa Khomasdal ni uwanja wa michezo unaopatikana huko Khomasdal, nchini Namibia. Ulitengenezwa mahususi kwa ajili ya michezo ya shule, kazi za makanisa na makundi ya vijana lakini umekuwa uwanja mkuu kwa idadi ya klabu za Namibia na unatumika zaidi na vilabu vikubwa kama vile Orlando Pirates F.C, United Africa Tigers F.C. Civics Windhoek, African Stars F.C. na Black Africa F.C.. Ulikuwa uwanja wa nyumbani wa klabu mbalimbali wakati uwanja wa Sam Nujoma Stadium, iliyoko Katutura, ilifungwa kwa matengenezo.

Mnamo mwaka 2009 magazeti ya Namibia yaliripoti kwamba uwanja huo haukuwa na choo wala sehemu maalum ya VIP na una sehemu ndogo sana ya kuegesha magari. Uwanja ulikuwa una milango miwili tu ya kutokea jambo ambalo lilikuwa la hatari.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Khomasdal Stadium a ticking time bomb The Namibian, 11 February 2009
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Khomasdal kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.