Uwanja wa michezo wa El Harti
Uwanja wa michezo wa El Harti ni uwanja wa michezo wa kihistoria wa jiji la Marrakech nchini Moroko. Uwanja huu upo eneo la Harti, katika mpaka wa wilaya za Guéliz na L'Hivernage. Hutumika mara nyingi katika michezo ya Soka. Uwanja wa Harti ni uwanja wa nyumbani wa timu ya mpira ya Kawkab de Marrakech. Una uwezo wa kujaza mashabiki takibani 20,000, kuacha na michezo ya timu ya Marrakech Kawkab mara kadhaa imekua ikitumika katika michezo ya timu ya Kadeti ya nchini Morocco. Uwanja huu una nyasi za bandia kuanzia mwanzoni mwa msimu wa 2008/2009.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Uwanja huu ulijengwa miaka ya 1930, wakati wa mradi wa maendeleo ya eneo la Harti ulioidhinishwa wakati huo na mamlaka husika. Ilitambulika rasi kama uwanja wa Marrakech katika miaka ya 1950, timu hii hapo kabla ilikua na makazi yake huko Marrakech Medina. Mnamo Disemba 2010, timu ya Marrakech ilihama kutoka uwanja wake pendwa na rasmimikaanza kutumia uwanja mpya wa Stade de Marrakech, iliyokua na uwezo wa kuingiza mashabiki 45000.
Ukarabati
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Septemba 2018, baada ya matengenezo kwa miezi kadhaa, uwanja huu ulifunguliwa rasmi kwa mara nyingine. Ukarabati huo uliogharibu takribani Dirham milioni 50 ulifanikisha kuwekwa nyasi asili, mitambo mipya ya kuangaza na kuweka namba katika viti vya washabiki.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa El Harti kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |