Uwanja wa Ndege wa Wilson (Kenya)
Uwanja wa Ndege wa Wilson uko kilomita tano kusini mwa jiji la Nairobi, Kenya, karibu na vitongoji vya Langata, South C na Kibera.
Uwanja huo wa ndege umekuwa ukitumika tangu 1933. Ulikuwa uwanja mkuu wa ndege hadi kufunguliwa kwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Uwanja huo wa ndege unatumika kwa safari za kimataifa pamoja na za ndani ya nchi. Inatumika zaidi na ndege ndogo. Sekta zinazotumia huduma zake sana ni za utalii, huduma za afya na kilimo. Uwanja huo wa ndege una wastani ya 120,000 ya ndege zinazoshuka na kupaa kwa mwaka. Airkenya na kampuni nyingine ndogo za ndege zinatumia uwanja wa Wilson kwa huduma za abiria za ndani ya nchi, badala ya Uwanja wa Jomo Kenyatta ambao ni uwanja mkuu wa ndege jijini Nairobi. Wamisionari wanaohudumu ndege kama AMREF, MAF na AIM AIR hutumia uwanja wa Wilson kama wigo wao wa Afrika. Uwanja huo wa ndege hutumiwa pia kwa mafunzo ya urubani. "Kenya Airports Authority" (KAA) viwanja vya Ndege ya Kenya ndio imedhibitiwa na mamlaka ya kuendesha uwanja huu wa ndege.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Uwanja huu wa ndege awali ulianzishwa mnamo mwaka wa 1933 kama Nairobi Aerodrome, na ulikuwa ukitumika kwa usafirishaji wa angani wa barua na shirika la ndege la Imperial. Uwanja huo mara ukabadilishwa jina kuwa uwanja wa ndege wa Wilson mwaka wa 1962. Uwanja huo umechukua jina la Bibi Florence Kerr Wilson, mmoja wa waanzilishi wa usafiri wa angani nchini Kenya.
Kampuni za Ndege na Sehemu za Usafiri
[hariri | hariri chanzo]Shirika la Sehemu ya Usafiri | Destination |
---|---|
Aero Kenya | Eldoret |
Airkenya Express | Amboseli, Kilimanjaro, Lamu, Lewa Downs, Malindi, Masai Mara, Meru, Mombasa, Nanyuki, Samburu |
ALS - Aircraft Leasing Services | Loki, Rumbek, Juba |
Blue Bird Aviation (Kenya) | |
Delta Connection (Kenya) | Juba, Yei, Rumbek |
Safarilink Aviation | Safarilink Aviation |
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Kenya Airports Authority, yaani Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Kenya -Uwanja wa Wilson
- Kamera ya Mtandao ya Moja kwa Moja ya Uwanja wa Wilson
- Klabu ya Aero ya Afrika Mashariki Archived 25 Novemba 2009 at the Wayback Machine.
- "Habari kuhusu uwanja wa ndege huko HKNW Archived 16 Mei 2011 at the Wayback Machine." katika World Aero Data. Data ni ya Oktoba 2006.. Source:"Habari kuhusu uwanja wa ndege huko DAFIF"
- "Habari kuhusu uwanja wa ndege huko HKNW" huko Great Circle Mapper. Asili:"Habari kuhusu uwanja wa ndege huko DAFIF" (mnamo Oktoba 2006).
- "Hali ya anga ya HKNW" huko Great Circle Mapper. Asili:"Habari kuhusu uwanja wa ndege huko DAFIF" (mnamo Oktoba 2006).
- "Historia ya ajali ya WIL Archived 29 Septemba 2007 at the Wayback Machine." ""Aviation Safety Network", yaani Mtandao wa Usalama wa Uurubani".
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Uwanja wa Ndege wa Wilson (Kenya) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |