Uwanja wa Ndege wa Kasane
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kasane ni uwanja wa ndege unaohudumia mji wa Kasane, katika Wilaya ya Chobe nchini Botswana. Uwanja wa huo wa ndege upo kando ya Barabara ya A33, kusini mwa mji huo na kusini mwa mpaka na Namibia.
Shirika la ndege la Botswana hutoa ratiba za huduma kati ya Kasane na Gaborone siku za Jumanne, Ijumaa, na Jumapili. Wafanyabiashara wengi wa ndege za charter hutoa ndege kwa vituo vingine vya karibu.
Kwa sababu ni karibu na Hifadhi ya Taifa ya Chobe, uwanja huu wa ndege hutumika zaidi kwa utalii. Nyumba nyingi za kulala wageni katika eneo la Kasane hutoa usafiri hadi uwanja wa ndege. Usafiri wa basi unapatikana kwa kusafiri kwenda katika maporomoko ya maji ya Victoria nchini Zambia na Zimbabwe.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kituo cha sasa kilifunguliwa tarehe 22 Februari 2018. Ilibadilisha jengo la awali la kituo ambacho kilifunguliwa mwaka 1991.[1]
Kasane VOR na ADF ziko kwenye uwanja wa ndege.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Unathi, Nkanjeni (2018-02-22). "PICS: Upgraded Kasane International Airport in Botswana ready to welcome visitors". Traveller24. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-04-03. Iliwekwa mnamo 2019-06-12.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)