Nenda kwa yaliyomo

Utamaduni wa Kitanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Utamaduni wa Kitanzania
Shanga za kimasai

Utamaduni ni mfumo wa maisha ya watu jinsi wanavyoishi na maendeleo yao kijamii, kiuchumi, kisiasa n.k.

Tanzania ni moja kati ya nchi zinazosifika duniani kwa kulinda maadili yao.

Kuna makabila yasiyopungua 120 ambayo yote hutunza mila na desturi zao kwa kiasi tofautitofauti.

Mambo yanayofanya Tanzania kutunza utamaduni wake ni haya: heshima iliyopo miongoni mwa jamii hii husaidia watu kuwa na maendeleo kwa sababu ya heshima hiyo.[1]

Nyingine ni utunzaji wa watoto, wazee, vijana pamoja na walemavu ambao wote ni mazao ya jamii ambapo kila mtu katika jamii hufunzwa kuwahudumia watu waliopo katika jamii yake.

Tatu ni mavazi ya heshima ambayo kila mtu anapaswa kuvaa na si mavazi yanayovunja maadili ya Taifa.

Uwajibikaji miongoni mwa wanajamii katika shughuli za kijamii ambazo husaidia kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla hivyo jamii ndiyo nguvu kazi katika nchi hasa nchini Tanzania.

  1. "Utamaduni na Urithi Wetu | Tanzania". tanzania.sil.org. Iliwekwa mnamo 2024-01-13.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utamaduni wa Kitanzania kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.