Usindikaji wa lugha ya asili
Usindikaji wa lugha ya asili au usindikaji lugha asili (kutoka kwenye Kiingereza: Natural Language Processing, NLP kwa kifupi) ni tawi la akili bandia linalojihusisha na kuzipa kompyuta uwezo kuelewa maandishi au maneno yanayotamkwa katika namna ile ile ambayo binadamu wanaweza. Usindikaji lugha asili unaunganisha isimu, takwimu pamoja na mitandao mipana ya neva bandia kuchakata lugha ya binadamu katika mtindo wa maandishi au sauti.
Usindikaji lugha asili unatumika kwenye programu za kompyuta zinazofasiri maandishi kutoka lugha moja kwenda nyingine, kutambua sauti za maneno, na kuunda muhtasari wa vifungu vya maneno. Usindikaji lugha asili unatumika pia kwenye mifumo mikubwa ya lugha, roboti za mazungumzo kama Bard na ChatGPT, roboti za utoaji huduma kwa wateja, biashara, na kuongeza tija kwa wafanyakazi. [1]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Usindikaji lugha asili ulianza miaka ya 1940, baada ya vita kuu ya pili ya dunia ukiwa na lengo la kuunda mashine kwa ajili ya kufasiri lugha moja kwenda nyingine, kazi hii ilikua ngumu tofauti na matumaini ya awali. Mpaka kufika mwaka 1958, watafiti wakubwa kama Noam Chomsky wakaanza kutambua udhaifu uliokuwepo kwenye mbinu za wakati huo za usindikaji lugha [2], Noam Chomsky aligundua kua, mifumo (kiingereza: models) ya usindikaji lugha asili ya wakati huo ilikosa uwezo wa kung'amua maana ya sentensi ukiacha sintaksi yake, kwa maneno mengine mifumo ya usindikaji lugha asili ya wakati ule ilikua na uwezo wa kutambua muundo wa kisarufi wa sentensi lakini haikua na uwezo wa kutambua maana ya hio sentensi. [3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "What is Natural Language Processing? | IBM". www.ibm.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-01-10.
- ↑ "NLP - overview". cs.stanford.edu. Iliwekwa mnamo 2024-01-10.
- ↑ "Colorless green ideas sleep furiously - wikidoc". www.wikidoc.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-01-10.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Usindikaji wa lugha ya asili kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |