Nenda kwa yaliyomo

Ushiriki wa Vijana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ushiriki wa vijana ni ushiriki kazi wa vijana katika jamii zao; mara nyingi ilitumika kama ufupisho wa vijana katika idara mbalimbali, ikiwemo kufanya maamuzi, michezo, shule na shughuli zozote ambazo kihistoria vijana walikuwa hawashiriki.

Uanzishwaji

[hariri | hariri chanzo]

Ushiriki wa vijana ulitumika na mawakala wa kiserikali, watafiti, wasomi, na wengineo kumaanisha na kutathimini ushiriki kazi wa vijana katika shule, michezo, serikali, maendeleo ya jamii na shughuli za kiuchumi.

Mnamo mwaka 1975, Tume ya taifa ya rasirimali ya vijana katika Umoja wa Mataifa wameelezea ushiriki kazi wa vijana kama: Ushiriki wa vijana ni uhusishwaji wa vijana katika uwajibikaji wa matendo ambayo yanaleta changamoto ambazo zinaleta mahitaji ya kweli, na nafasi za kupanga na/au kufanya maamuzi yanayoathiri wengine katika shughuli ambazo matokeo yake yanawaathiri vijana na wengineo.

Mnamo mwaka 1995, Chama cha afya ya akili ya watu wa Kanada (CMHA) walianzisha ufafanuzi maana ushiriki kazi kama: Inamaanisha ushiriki wa vijana inahusisha utambuzi na kulea nguvu za vijana, matamanio, na uwezo wa vijana kupitia nafasi halisi ili vijana waweze kujihusisha na maamuzi ambayo yatawaathiri kila mmoja. Katika mwaka 2006 Jumuiya ya madola ya programu ya vijana na UNICEF waliyatambua.