Upostulanti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Upostulanti (kutoka neno la Kilatini "postulare", yaani kuomba) ni hatua ya awali katika safari ya malezi utawani.

Kwa kawaida unatangulia hatua ya unovisi.

Mpostulanti amekaribishwa jumuiani ili aone zaidi maisha yalivyo na upande wake watawa waone tabia na nia zake zilivyo.

Urefu wa muda wa upostulanti (miezi au miaka) unategemea sheria za shirika, maendeleo ya mhusika n.k.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Upostulanti kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.