Umoja: Kijiji ambacho wanaume ni marufuku
Umoja: Kijiji ambacho wanaume ni marufuku ni filamu ya makala ya Ufaransa kuhusu kijiji cha Umoja kilichopo nchini Kenya, iliyoongozwa na Jean Crousillac na Jean-Marc Sainclair na kutolewa mnamo 2009.
Muhtasari
[hariri | hariri chanzo]Tangu 1970 hadi 2003, mamia ya wanawake wanadai kuwa wamebakwa na askari wa jeshi la Uingereza kaskazini mwa Kenya. Wakishutumiwa kuleta aibu kwenye jamii yao, wengi wao walipigwa na kukataliwa na wanaume wao. Baadhi ya wanawake walianzisha kijiji chao ambacho walikipa jina la Umoja ambacho kilikuwa cha wanawake pekeyao na kuwa kimbilio la wanawake wengi wa Sumburu. Maendeleo ya kijiji cha umoja ya yalisababisha wivu kwa wanaume na kupelekea uvamilizi wa mara kwa mara na kushabisha matatizo kwa mwasisi wa kijiji icho, Rebecca Lolosoli.
Tuzo na uteuzi wa tamasha
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 2009, filamu hii ilishinda tuzo ya Fedha katika tuzo za FIPA katika kategoria ya Hadithi Kubwa na Matukio ya Kijamii.[1].[2] Pia ilishinda tuzo la Msalaba Mwekundu katika tamasha la Kimataifa la Filamu la Reykjavíki.[3]
Mwaka 2009 ilichaguliwa na matamasha ya kimataifa ya filamu yafuatayo:
- Tamasha la Kimataifa la Filamu na Jukwaa la Haki za Kibinadamu (Geneva, Uswisi)
- Tamasha la Kimataifa la Filamu la Jean Rouch (Paris, Ufaransa)
- Tamasha la Kimataifa la Filamu za makala(Thessaloniki, Ugiriki)
- Tamasha la Filamu la Ecovision (Palermo, Italia)
- Tamasha la Doc-Cévennes (Lasalle, Ufaransa)
- Tamasha la Kimataifa la Filamu za makala na Anthropolojia (Pärnu, Estonia)
- Tamasha la Filamu za makala ya Haki za Kibinadamu - Filamu ya ufunguzi (Glasgow, Scotland)
- Tamasha la Kimataifa la Filamu la Kusini mwa Appalachi (Tennessee, Marekani)
- Tamasha la Uhuru (Brussels, Ubelgiji)
- Tamasha la Kimataifa la Filamu la Flahertania (Perm, Urusi)
- Tamasha la Kimataifa la Filamu la Flahertania (Perm, Urusi)
- Tamasha la Ethnografia la Rio (Rio de Janeiro, Brazili)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Sistach, Dominique (2011). "« Interdit aux enfants et aux chiens »". Le sociographe. n° 34 (1): 45. doi:10.3917/graph.034.0045. ISSN 1297-6628.
{{cite journal}}
:|volume=
has extra text (help); no-break space character in|title=
at position 2 (help) - ↑ "UMOJA, LE VILLAGE INTERDIT AUX HOMMES", Le Monde.fr (kwa Kifaransa), 2011-08-06, iliwekwa mnamo 2022-08-09
- ↑ https://www.mbl.is/media/34/1734.pdf
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Umoja: Kijiji ambacho wanaume ni marufuku kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |