Ukukwi-miti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ukukwi-miti
Ukukwi-miti zumaridi (Hapsidophrys smaragdina)
Ukukwi-miti zumaridi (Hapsidophrys smaragdina)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Colubridae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri)
Oppel, 1811
Nusufamilia: Colubrinae
Ngazi za chini

Jenasi 2, spishi 5:

Kukwi-miti ni spishi za nyoka za jenasi Hapsidophrys na Rhamnophis katika familia Colubridae.

Nyoka hawa ni warefu kiasi: kwa wastani sm 70-100 na kipeo cha m 1.1-1.3 kulingana na spishi. Wanafanana na kukwi lakini magamba ya mgongo ya spishi za Hapsidophrys yana miinuko na macho ya spishi za Rhamnophis ni makubwa zaidi. Magamba ya tumbo ya spishi zote yana miinuko pia inayosaidia nyoka hawa kupanda juu ya miti. Rangi yao ni kijani mara nyingi pamoja na madoa au mistari myeusi.

Kukwi-miti huishi mitini ambapo huwinda mijusi na vyura.

Kukwi-miti hawana sumu na hawang'ati kwa kawaida. Hutegemea rangi yao kama majificho (au kamafleji) na wakitishwa hujaribu kutoroka. Shingo ya spishi za Rhamnophis inafura wakitegwa.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukukwi-miti kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.