Nenda kwa yaliyomo

Ukosefu wa ajira kwa vijana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ukosefu wa ajira kwa vijana ni hali ya vijana wanaotafuta kazi, lakini hawapati, wenye umri wa miaka 15 hadi 24, uliobainiwa na Umoja wa Mataifa. Mtu ambaye hajaajiriwa anatambulika kama mtu ambaye hana kazi lakini ana bidii ya kutafuta kazi. Ili aweze kutimiza vigezo na malengo kuwa na ajira kwa kipimo rasmi na cha takwimu, ni lazima awe ana ajira, utayari na uwezo wa kufanya kazi uliyo rasmi ni "umri wa kufanya kazi" (mara nyingi ni vijana hadi miaka 60), bado wanabidi kutafuta nafasi. Viwango vya ukosefu wa ajira kwa vijana ni kubwa ukilinganishwa na watu wazima kwa kila Nchi.

Ukosefu wa ajira kwa vijana umeelezwa kuwa mkubwa,kama sio kichochezi cha msingi kwa ajili ya mapinduzi, kisiasa na msukosuko wa kijamii, migogoro dhidi ya mfumo na serikali. Kihistoria imeusishwa na machafuko na mabadiliko au kupinduliwa kwa uanzishwaji wa kisiasa na mabadiliko makubwa ya kijamii, na migogoro kama vile mapinduzi ya kiarabu, vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Urusi na mapinduzi ya Ufaransa yote kwa kiasi kibwa yanayosababishwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kwa vijana.[1]

Kuna vijana bilioni 1.2 Duniani wenye miaka kati ya 15 hadi 24, hesabu ya asilimia 17 ya idadi ya vijana Duniani. Asilimia 87 wanaishi kwenye nchi zinazoendelea. Kiwango cha umri kinachofafanuliwa na Umoja wa Mataifa kinazungumziwa ni kipindi ambacho shule ya lazima ina isha hadi umri wa miaka 24. Ufafanuzi huu bado una utata kwani sio tu unaathiri takwimu za ukosefu wa ajira lakini pia una jukumu muhimu katika ufumbuzi unaolengwa, uliondwa na watunga sheria ulimwenguni.

Mijadala mikuu miwili inaendelea leo. Kwanza, kufafanua umri wa vijana si dhahiri kama inavyoonekana. Mitazamo miwili ya kinadharia inatawala mjadala huu. Ujana unaweza kuonekana kama hatua katika maisha kati ya ujana na utu uzima au kama kikundi kilicho jengwa na utamaduni wake mdogo, na kufanya vigumu kuanzisha anuwai ya umri unaofanana kati ya nchi. Pili, ufafanuzi wa ukosefu wa ajira ambao unasababisha uwezekano wa kutohesabu baadhi ya vijana walioachwa kazini. Wale ambao hawana kazi na hawatafuti kazi kikamilifu - mara nyingi ni wanawake - wanachukuliwa kama wasiyo fanya kazi na hivyo kutengwa katika takwimu za ukosefu wa ajira. Kujumuishwa kwao kungeongeza kwa kiasi kikubwa kiwango cha ukosefu wa ajira.

  1. Rasmussen, Jacob (2010-07-20). "Mungiki as youth movement". YOUNG. 18 (3): 301–319. doi:10.1177/110330881001800304. ISSN 1103-3088.