Ukiki
Mandhari
Ukiki | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 2
|
Ukiki au pundamakaa ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Ceuthmochares katika nusufamilia Phaenicophaeinae ya familia Cuculidae wanaofanana na kekeo. Wana mnasaba na malkoha wa Asia. Wanatokea misitu wa Afrika kusini kwa Sahara. Rangi yao ni buluu au kijani na wana domo njano (kwa sababu ya hii huitwa yellowbill kwa Kiingereza). Hula wadudu wakubwa hasa lakini konokono, vertebrata wadogo, matunda na mbegu pia. Kinyume na kekeo hutengeneza tago lao lenyewe katika mti. Jike hutaga mayai meupe mawili.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Ceuthmocharis aereus, Ukiki Buluu (Chattering yellowbill)
- Ceuthmocharis a. aereus, Ukiki buluu
- Ceuthmocharis a. flavirostris, Ukiki Magharibi
- Ceuthmocharis australis, Ukiki Kijani (Whistling yellowbill)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Ukiki buluu