Nenda kwa yaliyomo

Malkoha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Malkoha
Malkoha uso-mwekundu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Cuculiformes (Ndege kama kekeo)
Familia: Cuculidae (Ndege walio na mnasaba na kekeo)
Nusufamilia: Phaenicophaeinae (Ndege wanaofanana na malkoha)
Ngazi za chini

Jenasi 8

Malkoha (kutoka Kisinhala: mal-koha au kekeo-maua) ni ndege wakubwa kiasi wa nusufamilia Phaenicophaeinae katika familia Cuculidae. Spishi za malkoha zinazotokea Afrika zinaitwa ukiki (Ceuthmochares) na kua (Coua) kwa Kiswahili. Lakini hivi karibuni wataalamu wengine wameainisha kua katika nusufamilia yao, Couinae, pamoja na kekeo-ardhi (Carpococcyx). Nje ya Afrika spishi zote zinatokea misitu ya Asia ya Kusini na ya Mashariki. Rangi za ndege hawa ni kijivu, kahawia au buluu, pengine nyeupe chini, na spishi nyingi zina nyekundu kwa tumbo, koo, uso, kishungi na/au domo. Spishi zinazotafuta chakula ardhini zina miguu yenye nguvu na zinaweza kukimbia. Zile zinazokaa mitini huenda kutoka tawi hadi tawi na kuruka kama dudumizi. Hula wadudu na vertebrata wadogo kama mijusi hasa lakini mbegu na beri pia. Kinyume na kekeo (Cuculinae) malkoha hutengeneza tago lao lenyewe katika mti kwa kawaida. Jike hutaga mayai 1-5 kufuatana na spishi.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Asia

[hariri | hariri chanzo]