Nenda kwa yaliyomo

Ujosefu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joseph II alivyochorwa na Anton von Maron, 1775.

Ujosefu (au Josefini) ni jina la sera za kiutawala za kaisari Yosefu II wa Austria miaka 1780-1790.

Sera hizo zilifuata falsafa ya mwangaza na kuingilia na kubana mamlaka ya Kanisa katika mambo mengi, hata madogo sana.

Kwa sababu hiyo alilaumiwa vikali na Kanisa Katoliki na kuhusianishwa na tapo la Wamasoni.

Pamoja na hilo, alipatwa na upinzani mkubwa, na hatimaye alifuta baadhi ya maamuzi yake.

Alipokufa, mdogo wake aliyemrithi, Leopoldo II, alizidi kurudisha mambo yalivyokuwa awali na kujali hisia za wananchi.

  • Berenger, Jean (1990), A History of the Habsburg Empire, 1700-1918, Edinburgh: Addison Wesley
  • Ingrao, Charles W. (2000), The Habsburg Monarchy, 1618-1815, New York: Cambridge University Press
  • Kann, Robert (1974), A History of the Habsburg Empire, 1526-1918, Los Angeles: University of California P
  • Okey, Robin (2002), The Habsburg Monarchy c. 1765-1918, New York: Palgrave MacMillan
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ujosefu kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.