Ugonjwa wa kutotulia kihisia
Ugonjwa wa kutotulia kihisia | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Tiba ya magonjwa ya akili |
Dalili | Mahusiano yasiyo na utulivu, hisia za kibinafsi, na na hisia mbalimbali; msukumo wa kuamua bila kufikiria; tabia ya kujiua mara kwa mara na kujidhuru; hofu ya kuachwa; hisia sugu ya utupu; hasira isiyofaa; kuhisi kujitenga na ukweliy[1][2] |
Miaka ya kawaida inapoanza | Utu uzima wa mapema[2] |
Muda | Muda mrefu[1] |
Visababishi | Si wazi[3] |
Sababu za hatari | Historia ya familia, kiwewe, unyanyasaji[1][4] |
Njia ya kuitambua hali hii | Kulingana na dalili zilizoripotiwa[1] |
Utambuzi tofauti | Matatizo ya utambulisho, matatizo ya hisia, matatizo ya baada ya kiwewe, matatizo ya matumizi mabaya ya madawa ya kulevya, ugonjwa wa hisia zisizo za kawaida, ugonjwa wa Narsisisti (kujipenda kupita kiasi), au ugonjwa wa tabia ya kijamii isiyo ya kawaida[2][5] |
Matibabu | Tiba ya maadili[1] |
Utabiri wa kutokea kwake | Inaboreka muda unavyosonga[2] |
Idadi ya utokeaji wake | 1.6% ya watu katika mwaka fulani[1] |
Ugonjwa wa kutotulia kihisia (kifupi kwa Kiingereza: EUPD; pia: Borderlne personality disorder, BPD, yaani Ugonjwa wa hali ya utu ya mpakani [6]) ni ugonjwa wa akili unaojulikana kwa muundo wa muda mrefu wa mahusiano yasiyo imara, hisia potovu za kujihusu, na athari kali za kihisia.[1][2][7] Watu binafsi mara nyingi hujihusisha na mambo ya kujidhuru na tabia nyinginezo hatari.[1] Wale walioathirika wanaweza pia kuhangaika na hisia ya utupu, hofu ya kuachwa, na kujitenga na ukweli.[1] Dalili zake zinaweza kuchochewa na matukio yanayochukuliwa kuwa ya kawaida kwa wengine.[1] Tabia hii kwa kawaida huanza katika utu uzima wa mapema na hutokea katika hali mbalimbali.[2] Matumizi mabaya ya dawa, unyogovu, na matatizo ya kula mara nyingi huhusishwa na ugonjwa huu.[1] Takriban 10% ya watu walioathiriwa hufa kwa kujiua.[1][2]
Sababu za ugonjwa huu haziko wazi, lakini zinaonekana kuhusisha sababu za kijeni, neva, mazingira na mambo ya kijamii.[1][3] Ugonjwa huu unatokea mara tano zaidi kwa mtu ambaye ana jamaa wa karibu aliyeathirika.[1] Matukio mabaya ya maisha yanaonekana pia kuuchangia.[4] Utaratibu wa kimsingi unaonekana kuhusisha mtandao wa mbele wa niuroni wa mfumo wa neva na miundo mingine katika ubongo inayodhibiti hisia zetu nyingi.[4] Ugonjwa wa hali ya utu ya mpakani unatambuliwa na Mwongozo wa Uchunguzi na Takwimu wa Matatizo ya Akili (DSM) kama ugonjwa wa utu, pamoja na matatizo mengine tisa kama hayo.[2] Utambuzi wake unategemea dalili, wakati uchunguzi wa kimatibabu unaweza kufanywa ili kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa matatizo mengine.[1] Hali hii lazima itofautishwe na tatizo la utambulisho au matatizo ya matumizi ya dutu, miongoni mwa uwezekano mwingine mwingi.[2]
Ugonjwa wa hali ya utu ya mpakani kwa kawaida hutibiwa kwa tiba, kama vile tiba ya utambuzi wa tabia (CBT) au tiba ya tabia ya mjadala wa kimantiki wa mawazo na maoni (DBT).[1] Mjadala huu wa kimantiki wa mawazo na maoni unaweza kupunguza hatari ya kujiua.[1] Tiba inaweza kutokea moja kwa moja au kwa kikundi.[1] Ingawa dawa hazitibu ugonjwa huu, zinaweza kutumika kusaidia kutibu dalili zinazohusiana nao.[1] Watu wengine wenye ugonjwa huu wanahitaji huduma ya hospitali.[1]
Takriban 1.6% ya watu huwa wana ugonjwa huu katika mwaka fulani, na makadirio mengine yanafikia 6%.[1][2] Wanawake hugunduliwa na maradhi haya mara tatu zaidi kuliko wanaume [2] na unaonekana kuwa chini ya kawaida kati ya watu wazee.[2] Hadi nusu ya watu huboreka katika kipindi cha miaka kumi.[2] Watu walioathirika kwa kawaida hutumia kiasi kikubwa cha rasilimali za afya.[2] Kuna mjadala unaoendelea kuhusu kuupa jina ugonjwa huu, hasa ufaafu wa neno mpaka.[1] Ugonjwa huu mara nyingi hunyanyapaliwa katika vyombo vya habari na uwanja wa magonjwa ya kiakili.[8]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 1.15 1.16 1.17 1.18 1.19 1.20 1.21 "Borderline Personality Disorder". NIMH. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 2.12 2.13 Diagnostic and statistical manual of mental disorders : DSM-5 (tol. la 5th). Washington, D.C.: American Psychiatric Publishing. 2013. ku. 645, 663–6. ISBN 978-0-89042-555-8.
- ↑ 3.0 3.1 Clinical Practice Guideline for the Management of Borderline Personality Disorder. Melbourne: National Health and Medical Research Council. 2013. ku. 40–41. ISBN 978-1-86496-564-3.
In addition to the evidence identified by the systematic review, the Committee also considered a recent narrative review of studies that have evaluated biological and environmental factors as potential risk factors for BPD (including prospective studies of children and adolescents, and studies of young people with BPD)
- ↑ 4.0 4.1 4.2 Leichsenring F, Leibing E, Kruse J, New AS, Leweke F (Januari 2011). "Borderline personality disorder". Lancet. 377 (9759): 74–84. doi:10.1016/s0140-6736(10)61422-5. PMID 21195251.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Borderline Personality Disorder Differential Diagnoses". emedicine.medscape.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Aprili 2011. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Borderline personality disorder NICE Clinical Guidelines, No. 78. British Psychological Society. 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 5 Agosti 2020.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Chapman, Alexander L. (Agosti 2019). "Borderline personality disorder and emotion dysregulation". Development and Psychopathology (kwa Kiingereza). 31 (3). Cambridge, England: Cambridge University Press: 1143–1156. doi:10.1017/S0954579419000658. ISSN 0954-5794. PMID 31169118. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Desemba 2020. Iliwekwa mnamo 5 Agosti 2020.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Aviram RB, Brodsky BS, Stanley B (2006). "Borderline personality disorder, stigma, and treatment implications". Harvard Review of Psychiatry. 14 (5): 249–56. doi:10.1080/10673220600975121. PMID 16990170.