Nenda kwa yaliyomo

Uche Mac-Auley

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uche Mac-Auley (alizaliwa Uchechukwu Nwaneamaka), pia aliyejulikana kama Uche Obi Osotule, ni mwandishi wa Nigeria, mtayarishaji wa sinema na mwigizaji mkongwe.[1]

Maisha ya awali na Elimu

[hariri | hariri chanzo]

Mac-Auley ametokea jimbo laDelta nchini Nigeria ambapo ni eneo la kijiografia lililo kusini-kusini mwa Nigeria iliyotawaliwa na makabila machache vile vile watu wa Igbo wa Nigeria. Wazazi wa Mac-Auley walikuwa walimu waliosafiri mara kwa mara hivyo Mac-Auley alitembea sana na hakukaa sehemu moja kwa muda mrefu kufanya Mac-Auley kuhudhuria shule nyingi za msingi lakini kuja kupata “Cheti cha Kwanza cha Kumaliza Shule” kutokea Shule ya Msingi ya Osoro na elimu ya shule ya sekondari katika shule ya Anglican Girls Grammar na Idia College ambapo alipata West African Senior School Certificate Examination|West African Senior School Certificate Examination Certificate. Mac-Auley alihitimu na shahada ya Kiingereza katika Delta State university.[2][3]

Mac-Auley anaweza kuelezwa kama mwigizaji mkongwe na mmoja ya waanzilishi wa tasnia ya sinema nchini Nigeria.[4] Mac-Auley alianza uigizaji wa sinema za Nigeria siku nyingi kabla ya uigizaji wa sinema za Nigeria ulivoboreshwa hivi leo.The Guardian (Nigeria)|Guardian print media ilimtambulisha Mac-Auley mwigizaji asiyekuwa na wakati na mwigizaji muhimu.[1] Mac-Auley alijadiliwa katika tasnia ya sinema za Nigeria kwa mara ya kwanza katika mfululizo wa vipindi vya Nigerian TV mwaka 1991 ilioitwa Checkmate (Nigerian TV series)|Checkmate ambayo ilitayarishwa na ilielekezwa marehemu mtayarishaji mkongwe Amaka Igwe ambapo aliigiza jukumu muhimu katika wasifu aliyeitwa Nkemji, “malkia wa urembo” wa kijiji na kuwashirikisha waigizaji wa Nollywood kama Richard Mofe-Damijo, Norbert Young, Francis Agu, Bimbo Manuel, Kunle Bamtefa, na Binta Ayo Mogaji. Katika kitabu kilichoitwa The Creation of Nigerian Film Genres, kilichoandikwa na mwandishi wa Marekani Jonathan Haynes, Mac-Auley alitajwa miongoni mwa sura za mapema kuonekana katika tasnia ya sinema za Nigeria kabla ya kuboreshwa na pia kama mwanzilishi wa tasnia ya sinema za Nigeria.[4] Mac-Auley alichukua mapumziko marefu katika uigizaji[5][6][7] kuwa mwandishi wa kitabu cha hadithi za watoto[8] lakini alirejea katika uigizaji mwaka 2016 ambako aliangaziwa katika sinema ilioitwa “Mid-Life”.[9]

Mac-Auley mbali na kuwa mwigizaji pia ni mwandishi wa vitabu vya hadithi za watoto, mwandishi wa hati za sinema na mtayarishaji wa sinema na ametayarisha sinema; Dangerous Twins, Sins of my Mother and In a Lifetime.[10]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Mac-Auley aliolewa mara mbili. Mwanzo, aliolewa na mtayarishaji wa sinema za Nollywood Obi Osotule ambaye alikutana nae mwaka 1993 katika uigizaji wa sinema iliyoitwa “Unforgiven Sin”. Mac-Auley alipeana talaka na Obi Osotule mwaka 2002. [3] na mwaka 2006 akaolewa na Solomon Mac-Auley.[11]

Mac-Auley aliingia katika tasnia ya sinema za Nigeria kwa jina la “Uche Osotule” ambaye “Osotule” lilikuwa jina la ukoo la mume wake kwa muda huo, kisha baada ya kuoana tena akabadili jina lake la mwisho kuwa “Mac-Auley” ambalo ndo jina la mwisho la mume wake wa sasa.[6]

Filamu zilizochaguliwa na vipindi vya TV

[hariri | hariri chanzo]
  • 5th Floor (2017) as Whenu
  • Mid Life (2016)
  • Images in the Mirror (2004) as Ada
  • Saving Alero (2001)
  • Thunderbolt: Magun (2001)
  • Obstacles (1998)
  • Another Love (1996)
  • Unforgiven Sin (1993)
  • Checkmate (Nigerian TV series)|Checkmate (1991) as Nkemji
  1. 1.0 1.1 "Uche Macauley: A loaded comeback for the timeless actress". guardian.ng (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-28. Iliwekwa mnamo 2019-12-28.
  2. Magazine, Yes International! (2016-10-11). "A FEW THINGS THAT WILL INTEREST YOU ABOUT ACTRESS UCHE MAC-AULEY". Yes International! Magazine (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-28. Iliwekwa mnamo 2019-12-28. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  3. 3.0 3.1 "Men can't kill my dream – Uche Mac-auley ". www.thenigerianvoice.com. Iliwekwa mnamo 2019-12-28.
  4. 4.0 4.1 Haynes, Jonathan (2016). Nollywood: The Creation of Nigerian Film Genres. University of Chicago Press. uk. 335. ISBN 022638795X.
  5. Tide, The. "Meet Veteran Nollywood Stars Missing In Action" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-12-28.
  6. 6.0 6.1 "Uche Mac-Auley Actress reveals reason for absence, says she's fully back to acting". www.pulse.ng. Iliwekwa mnamo 2019-12-28.
  7. Atoyebi, Abiola (2016-10-18). "How time flies! 18 favorite Nollywood actors we miss on screen". www.legit.ng (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-28. Iliwekwa mnamo 2019-12-28. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  8. "Uche Mac-Auley's 'Next Uche Mac-Auley's 'Next Chapter'". Vanguard News (kwa American English). 2017-11-27. Iliwekwa mnamo 2019-12-28.
  9. "Uche Mac-Auley Actress returns to Nollywood, stars in "Mid Life"". www.pulse.ng. Iliwekwa mnamo 2019-12-28.
  10. "Actress reveals reason for absence, says she's fully back to acting". Pulse Nigeria (kwa American English). 2016-02-26. Iliwekwa mnamo 2020-05-27.
  11. "#Why Uche's hubby Solomon Mac-Auley is every woman's dream". The Nation Newspaper (kwa American English). 2018-03-09. Iliwekwa mnamo 2019-12-28.