Francis Agu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Francis Agu (18 Februari 196520 Machi 2007) alikua muigizaji na mtangazaji wa televisheni kutoka Nigeria. Alikuwa maarufu katika mfululizzo wa filamu za televisheni kwa jina la Checkmate.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Francis Okechukwu Agu alizaliwa jijini Lagos Februari 18, 1965 katika familia ya Kikatoliki ya Fidelis na Virginia Agu kutokea Enugu-Ngwo, jimbo la Enugu, alikuwa mtoto wa saba kati ya nane. Jina la Okechukwu, lina maana ya "fungu la Mungu”.[1]

Kijana mpole na mwenye akili, alikua mtumishi wa altareni katika kanisa la kikatoliki la Mt. Dominic lililopo Yaba, Lagos. Alianza elimu yake Ladi-Lak Institute Alagomeji, Ebute-Metta, Lagos. Elimu yake ya sekondari ya juu aliipata katika shule ya St. Finbarr's College, Lagos. Alisoma pia Chuo Kikuu cha Lagos, ambapo alisoma mawasiliano ya uma.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Kazi ya uigizaji ya Agu ilianza katika jumba la sanaa katika kanisa la Mt. Dominic, wakati huo alikua ayari akifanya kazi benki huko Lagos. Yodrac, iliyofadhiliwa na George Eboka, ilizalisha wasanii wengi tofauti kama Toyin Oshinaike, Kevin Ushi, Kris Ubani-Roberts, Williams Ekpo, Gregory Odutayo, Jude Orhorha, Tunji Otun, na Neye Adebulugbe. Kipaji cha Agu kilionekana mapema sana na mkurugenzi wa Yodrac kipindi hicho, Isaac John.

Alionekana kwa mara ya kwanza katika onyesho la This is Our Chance ya James Ene Henshaw, iliongozwa na Isaac John. Alicheza kama mhusika mkuu kwa jina la, King Damba. Maonyesho mengine yalijumuisha The Gods Are Not to Blame ya Ola Rotimi, na Trials of Brother Jero ya Wole Soyinka.

Segun Ojewuyi alimuongoza katika onyesho la The Man Who Never Died katika ukumbi wa michezo wa taifa jijini, Lagos. Hii ilifuatiwa na maonyesho mengine mbalimbali pamoja na waigizaji wengine wakomau kama vile Chuck Mike. Alipata nafasi kua katika kikundi cha muziki cha Steve Rhodes Voices, chini ya mkubwa wao bwana Steve Rhodes.

Agu alishiriki katika telenovela kwa jina la Checkmate, iliyochezwa katika miaka ya 1990 ambapo alicheza kama mhusika kwa jina la Benny. Alishiriki pia kama Ichie Million kaika filamu ya Living in Bondage, ambayo ilimpatia umaarufu sana. Alitengeneza filamu yake ya kwanza kwa jina la Jezebel mwaka 1994 na kuendelea kuigiza na kutengeneza filamu nyingi tofauti kama vile In the Name of the Father, A Divine Call, The Boy is Mine, Body and Soul, Love and Pride, A Dance in the Forest, na Take Me to Jesus.

Agu alianza kuugua Oktoba 2006, aliaga dunia tarehe 20 Machi 2007.

Filamu[hariri | hariri chanzo]

  • Living in Bondage (1992)
  • Bloodbrothers
  • Bloodbrothers 2
  • A Minute to Midnite
  • Untouchable
  • Circle of Doom (1993)
  • Jesus
  • Blood Money (1997)
  • Father of the Pride

Marejeo[hariri | hariri chanzo]