Uche Jombo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Uche Jombo Rodriguez (amezaliwa Abiriba, Jimbo la Abia, Nigeria, Disemba 28, 1979), ni mwigizaji, mwandishi na mtayarishaji wa filamu wa Nigeria.

Maisha ya zamani[hariri | hariri chanzo]

Uche Jombo ni mhitimu wa Hisabati na Takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Calabar na Programu ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Shirikisho cha Teknolojia Minna . Aliwahi kuolewa na Mmarekani anayeitwa Kenny. [1]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Uche Jombo alijitosa katika tasnia ya sinema ya Nigeria mwaka wa 1999 katika filamu ya Visa to Hell . Akiwa msanii wa filamu za bongo ameandika na kuandika pamoja filamu kadhaa ambazo baadhi yake ni pamoja na: The Celebrity, Games Men Play, Girls in the Hood & A Time to Love. Jombo aliendelea kutengeneza filamu kama vile Nollywood Hustlers, Holding Hope na kazi yake ya Damage ambayo inahusu masuala ya ukatili majumbani. Jombo ni balozi wa Globacom . [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Glo Ambassadors - Uche Jombo. Globacom Limited. Jalada kutoka ya awali juu ya 26 September 2011. Iliwekwa mnamo 28 September 2011.
  2. Celebrity crush (en-US). Punch Newspapers. Iliwekwa mnamo 2020-07-25.
Biofilm.png Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uche Jombo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.