Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1860

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1860 ulikuwa wa 19 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 6 Novemba. Upande wa "Republican Party", Abraham Lincoln (pamoja na kaimu wake Hannibal Hamlin) aliwashinda mgombea wa "Democratic Party" wa Kusini John Breckinridge (pamoja na kaimu wake Joseph Lane), mgombea wa "Democrats" wa Kaskazini Stephen Douglas (pamoja na kaimu wake Herschel Johnson) na mgombea wa "Constitutional Union" John Bell (pamoja na kaimu wake Edward Everett).

Matokeo[hariri | hariri chanzo]

Lincoln akapata kura 180, Breckinridge 72, Douglas 12 na Bell 39. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.