Kupoza kwa hewa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ubaridi hewa)
Pezi za kupoza zinaongeza uso wa kitu chenye joto

Kupoza kwa hewa ni njia ya kutawanya joto mahali pasipotakiwa. Uso wa kitu chenye joto unapitishiwa hewa iliyo na jotoridi ndogo zaidi.

Kunatumiwa katika injini ya mwako ndani, injini ya umeme, vifaa vya kielektroniki, kwa mfano kompyuta, na pia kwa utunzaji wa vyakula.

Injini inaweza kuharibika kutokana na upanuzi wa sehemu zake penye joto kali, katika vifaa vya umeme joto kali linaweza kuharibu nyaya na vifaa ndani yake (kapasita, vidukizi, vikinza n.k.). Kupunguza jotoridi ya vyakula juu ya sentigredi 0 kunachelewesha pia bakteria na mabadiliko yanayoweza kuharibu vyakula.

Kupoza kwa hewa kunatekelezwa kwa kuongeza uso wa kitu chenye joto, kwa kuongeza mwendo wa hewa juu ya uso wake au kwa kuunganisha mbinu hizo.

Katika utarakilishi, kupoza kwa hewa ni mfumo unaotumika ili kupepelea vijenzi ndani ya tarakilishi. Kwa mfano kipepeo tarakilishi ni mfumo wa kupoza kwa hewa.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.