Uandishi wa barua ya simu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Barua ya simu iliyotumwa na Orville Wright kwa baba yake mnamo Desemba 1903 kutoka Kitty Hawk, North Carolina, baada ya kufaulu kuruka kwa ndege.

Uandishi wa barua ya simu ni njia mojawapo ya mawasiliano ya haraka baina ya watu. Waandikiwa hupata taarifa haraka ukilinganisha na barua za kawaida, pia taarifa zake ni fupi na zina ujumbe unaoeleweka. Ufupi huo hutokana na gharama kubwa za malipo kwa sababu gharama ya simu ya maandishi hulipwa kulingana na idadi ya maneno mwandishi aliyoyaandika.

Pia barua za simu zipo za aina tatu ambazo ni:

  • 1, barua ya simu ya kawaida
  • 2, barua ya simu ya haraka na
  • 3, barua ya simu ya kupeleka fedha.

Mambo ya kuzingatia wakati wa uandishi ni:

  • 1, anwani ya mpeleka taarifa
  • 2, taarifa au ujumbe
  • 3, jina la mwandishi.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uandishi wa barua ya simu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.