Nenda kwa yaliyomo

Tyra Banks

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tyra Banks

Tyra Banks
Amezaliwa Tyra Lynne Banks
4 Desemba 1973
Marekani
Kazi yake ni mwigizaji, mwanamitindo, mfanyabiashara na mwimbaji nchini Marekani

Tyra Lynne Banks (alizaliwa 4 Desemba 1973) ni mwigizaji, mwanamitindo, mfanyabiashara na mwimbaji nchini Marekani.[1][2][3] Alipata umaarufu kama mwanamitindo alipokuwa kwenye miji ya Paris, Milan, London, Tokyo na New York. Banks ni mbunifu na mtangazaji mkuu wa kipindi cha America's Next Top Model. Yeye pia ni mbunifu wa True Buauty na mtangazaji wa kipindi cha mahojiano cha The Tyra Banks Show.

Maisha yake

[hariri | hariri chanzo]

Tyra Banks alizaliwa mjini Inglewood, California; mwana wa Carolyn na Donald Banks.[4] Wazazi wake waliachana pindi Tyra alipokuwa na miaka sita. Baadaye, Carolyn aliolewa na Clifford Johnson. Banks alisoma katika shule ya John Burroughs iliyopo mjini Los Angeles na kisha akaenda katika shule ya upili ya Immaculate Heart.

Kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

Mwanamitindo

[hariri | hariri chanzo]

Tyra alianza uanamitindo alipokuwa darasa la 11.[5] Baadaye, alienda mjini Paris kwa ajili ya kufanya kazi hii. Katika wiki yake ya kwanza mjini Paris, Tyra alipata umaarufu na mafanikio yaliyovunja rekodi kwani ilikuwa mwanzo wake katika uanamitindo. Yeye alishirikiana Anna Sui, CoverGirl, Badgley Mischka, Bill Blass, Chanel, Christian Dior, Dolce & Gabbana, H&M, McDonald's, Pepsi, Nike, Victoria's Secret na Yves Saint Laurent. Yeye ameonekana kwenye majalada maarufu kama Vogue, Harper's Bazaar, Cosmopolitan na Elle. Mnamo 1997, Tyra alipokea tuzo la VH1 Award for Supermodel of the Year. Mwaka huo huo, yeye alikuwa Mwamerika mweusi wa kwanza kutokea kwenye kasha ya jalada la Victoria's Secret.[6]

Filamu na televisheni

[hariri | hariri chanzo]

Banks alianza kuigiza kwenye msimu wa nne wa kipindi cha The Fresh Prince of Bel-Air ambapo aliigiza kama Jackie Ames. Aliigiza kwenye vipindi kama Felicity, MADtv na The Price Is Right

Hivi sasa yeye ana kipindi cha mahojiano cha The Tyra Banks Show, kilichoanza mnamo 12 Septemba 2005. Vilevile, yeye ni hakimu kwenye kipindi cha America's Next Top Model. Mnamo 2008, Banks alishinda tuzo la Daytime Emmy Award kwa kazi yake kwenye The Tyra Banks Show.

Banks amesema kuwa ataigiza kama Ursula Nyquist kwenye kipindi cha Gossip Girl msimu wa tatu.

Banks ameonekana kwenye video za muziki kama "Black or White" ya Michael Jackson, "Love Thing" ya Tina Turner na kwenye wimbo wa "Too Funky" ya George Michael.

Film
Mwaka Filamu Aliigiza kama Maelezo
1995Higher LearningDeja
1999Love StinksHolly Garnett
2000Love & BasketballKyra Kessler
Life-SizeEve Doll
Coyote UglyZoë
2002Halloween: ResurrectionNora Winston
Eight Crazy NightsVictoria's Secret GownSauti yake pekee
2007Mr. WoodcockMwenyewe
2008Tropic ThunderMwenyewe
2009Hannah Montanamwenyewe[7]
Vipindi
MwakaKipindiAliigiza kamaMaelezo
1993The Fresh Prince of Bel-AirJackie Ames

Aliigiza kwenye vipindi vifuatavyo:

  • Where There's a Will, There's a Way: 1
  • All Guts, No Glory
  • Father of the Year
  • Blood Is Thicker Than Mud
  • Fresh Prince After Dark
  • Take My Cousin... Please
  • You've Got to Be a Football Hero
1999 FelicityJane Scott

Aliigiza kwenye vipindi vifuatavyo:

  • A Good Egg
  • Kissing Mr. Covington
  • One Ball, Two Strikes
Just Shoot Me!Mwenyewe

Aliigiza kwenye vipindi vifuatavyo:

  • Nina Sees Red: 1
  • Nina Sees Red: 2
2000MADtvKatisha Latisha Parisha Farisha Johnson
  • Kipindi #5.17
  • Kipindi #5.25
2003-hadi leoAmerica's Next Top ModelHakimuTyra ni hakimu na mtunzi wa kipindi hiki
2004American DreamsCarolyn Gill
All of UsRoni
2005-2010The Tyra Banks ShowMtangazajiKipindi cha mahojiano
2009Gossip GirlUrsula Nyquist
  1. Jason Clark (2008). "Tyra Banks:Biography on MSN". MSN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-02. Iliwekwa mnamo 2008-07-18. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  2. "ABC News: Tyra Banks Experiences Obesity Through Fat Suit".
  3. "Tyra Banks On It - Forbes.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-12. Iliwekwa mnamo 2010-01-29.
  4. "Tyra Banks Biography". FilmReference.com.
  5. Hirschberg, Lynn (1 Juni 2008). "Banksable". New York Times.
  6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-09. Iliwekwa mnamo 2012-07-09.
  7. "'Hannah Montana' Film Scenes Shot In Cool Springs Mall". NewsChannel 5.com. 2008-05-28. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-29. Iliwekwa mnamo 2010-01-29.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]