Tupa (nyoka)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tupa
Tupa mdogo mweusi (Gonionotophis nyassae)
Tupa mdogo mweusi (Gonionotophis nyassae)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Lamprophiidae (Nyoka walio na mnasaba na chata)
Fitzinger, 1843
Nusufamilia: Lamprophiinae (Nyoka wanofanana na chata)
Fitzinger, 1843
Jenasi: Gonionotophis
Boulenger, 1893
Ngazi za chini

Spishi 15:

Tupa ni spishi za nyoka za jenasi Gonionotophis katika familia Lamprophiidae. Wamepewa jina hili kwa sababu mwili wao una umbo wa tupa yenye pande tatu.

Nyoka hawa ni wafupi hadi warefu kiasi, kati ya sm 30 na 160. Kichwa cha spishi ndefu kinafanana na kile cha kambare. Kwa kawaida rangi yao ni nyeusi, kijivu au kahawia. Tupa kusi anaweza kuwa na mlia mweupe mgongoni.

Tupa huenda polepole na kuwinda usiku. Hula amfibia na watambaachi, ikijumuisha hata nyoka wengine.

Nyoka hawa hawana sumu na kwa kawaida hawang'ati wakishikwa na watu.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tupa (nyoka) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.