Nenda kwa yaliyomo

Tungamo ya Jua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ulinganifu wa masi za nyota: nyota kibete nyekundu (M 0.1), Jua, nyota kibete buluu (M 8) na R136a (M 300)

Tungamo ya Jua (ing. Solar mass) inataja tungamo ya Jua letu ambayo ni takriban kilogramu 1.99 × 1030 . Hii inalingana na tungamo ya Dunia yetu mara 332,946.

Kiwango hiki hutumiwa kama kizio katika sayansi ya astronomia kwa kutaja tungamo ya magimba kwenye anga ya nje hasa nyota, fungunyota na galaksi.

Nyota nyingi huwa na tungamo baina ya x0.1 na x10 ya tungamo ya Jua. Mara chache kuna nyota kubwa sana yenye tungamo x250 za Jua. Hivyo Jua letu liko kwenye wastani wa tungamo za nyota kati ya nyota za safu kuu.

Ilhali tungamo ya Jua inaendelea kupungua polepole kutokana na mnururisho na upepo wa Jua kuna ufafanuzi wa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia wa kuhesabu tungamo ya Jua kuwa kilogramu 1.9891×1030[1].

Alama yake ni M ambako "M" inamaanisha "tungamo" na ☉ ni ishara ya Jua.

Vizio vinavyolingana

Tungamo moja ya Jua inalingana na

  • 27,068,510 x tungamo ya Mwezi M
  • 332,946 x tungamo ya Dunia M
  • 1,048 x tungamo ya Mshtarii M.

Njia Nyeupe (galaksi yetu) ina takriban milioni 180 tungamo za Jua ambayo inalingana na kilogramu 3.6 · 1041.


Marejeo

  1. Measuring the Universe - The IAU and astronomical units, tovuti ya Ukia, iliangaliwa Novemba 2017